
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Naibu Waziri wake Mhe. Annastazia James Wambura walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akishangilia mara baada ya Donald Ngoma kuiandikia Yanga bao la kwanza mnamo Dakika ya 38 ya mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mhe. Venance Mwamoto akifuatilia mchezo kati ya Yanga Afrika na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
No comments:
Post a Comment