Sunday, January 17, 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE AONYA VYOMBO VYA HABARI NCHINI


Wamiliki wa vyombo habari,wahariri,waandishi na watangazaji wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ili kujenga heshima ya tasnia hiyo na kulinda amani ya nchi yetu.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi wa Serikali wa kulifuta kabisa Gazeti la Mawio linalochapishwa na Kampeni ya Mwanahalisi.

Waziri Nape alisema kuwa Serikali katika kuhakikisha inalinda na kusimamia sheria za nchi na Katiba imeamua kulifuta kabisa gazeti hilo kutoka katika daftari la msajili wa Magazeti ambapo amri hiyo imetolwa kwa tangazo la Serikali namba 55 lililotolewa Januari 15 mwaka huu.


Amesema kuwa uamuzi huo umetolewa kwa mujibu wa sheria ya Magazeti sura ya 229 kifungu cha 25(1) na kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya kielectroniki na posta sura 306 inazuia gazeti hilo kuchapishwa katika njia nyingine yeyote ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii (On line Publication).

"Serikali kwa masikitiko makubwa imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hili usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani ,utulivu,na usalama wa nchi yetu."anaelezaWaziri Nape

Aidha alisema kuwa hatua ya kulifuta gazeti hilo limechukuliwa baada ya msajili wa magazeti kufanya juhudi kubwa na za muda mrefu kuazia juni 2013 hadi januari 2016 za kumtaka mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habri na Makala zake bila mafanikio kila alipotakiwa kutoa maelezo alikuwa na majibu ya hovyo kejeli,na dharau yanayoashiria kama hakuna Serikali.

Pia alisema kuwa anatambua kuwa yeye ni mlezi wa vyombo hivyo lakini haimaanishi makosa kuwa atakuwa anakumbatia makosa kwani lazima itambuliwe kuwa yeye aliapa kuilinda Katiba ya Tanzania ambayo msingi wake ni amani na utulivu katika nchi.

Amesema kuwa makosa ambayo yamefanywa na gazeti hilo mengi kwani tangu mwaka 2013 wamekuwa wakifanya makosa na kuandikiwa barua za kuwaonya na wakati mwingine kutakiwa kupeleka ushahidi wa wanachokiandika lakini waalikuwa wanahaidi na kupuuzia.

Ameongeza kuwa ukiachilia mbali makosa ya huko lakini kwa hivi majuzi tu gazeti hilo lilichapisha habari ya kusema Machafuko Zanzibar kitendo ambacho ni uchochezi na kinahatarisha hali ya usalama nchini mwetu.

"msajili wa magazeti alitoa ushauri mara nane juu ya utendaji wa gazeti hili lakini hawakuweza kujirekebisha mfano mwingine gazeti limewahi kutangaza kuwa Maalim Seif ndiye rais wa Zanzibar jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi na ni hatari hivyo tunasema hakuna aliye juu ya sheria."anaeleza Waziri Nape

Amesema kuwa kuna magazeti mengi ambayo yalikuwa yanaachapisha habari ambazo hana afya kwa nchi yetu yaliwahi kufungiwa na kuonywa na baadaye yanajirekebisha lakini pia kuwa mstari wa mbele kuomba radhi tofauti na gazeti hilo ambalo limekuwa kiburi na kuendelea kukiuka sheria na maadili ya uandishi wa habari.

Pia amesema kuwa Serikali inasisitiza kuwa itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili,uweledi na sheria za nchi na kwamba itaendelea kutoa ushirikiano vyombo vyote vya habari na hiyo nikutokana nakutambua umuhimu wake.

Aidha katika hatua nyingine Waziri Nape amevipongeza vyombo vya habari vinavyozingatia maadili,uweledi na sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi huku akivitaja baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliwahi kuonywa na kujirekebisha kuwa ni Mwananchi,Mtanzania,The East African,Magazeti ya Daily News, Habari leo,Uhuru,na mengineyo.



Baadhi ya Waandhishi wakifuatilia kwa makini mkutano huo leo Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment