Taarifa zaidi zinasema Marehemu Mr Sukeiman aliamka asubuhi akamwambia mke wake hajiskii vizuri, lakini alienda baharini kuogelea kama kawaida yake.
Walikuwa wawili na mwenzie, wakaenda mbali sana wakati wa kirudi aliishiwa nguvu, alijitahidi akafika nchi kavu akiwa hoi kabisa amekunywa maji wengi na akawa anatokwa na mapovu mdomoni. Alifariki njiani akipelekwa hospitali.
Msiba upo upanga nyuma ya jeshi (Ngome) saa hii maiti imefuatwa wanakuja kuaga hapa nyumbani, mwili utarudi msikitini saa tisa kisha kuzika makaburi ya Kisutu nyuma ya chuo cha CBE. Apumzike kwa Amani.
No comments:
Post a Comment