Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Simba, Betram Mombeki (PICHANI, AKIWA NA UZI WA JTK RUVU) amejiunga na JKT Ruvu Stars ya Pwani. Mombeki amejiondoa Simba kwa sababu hakuwa
anaelewa atima yake katika klabu hiyo. Pamoja na kuonyesha uwezo wa kuridhisha akiwa Simba msimu
uliopita, Mombeki alijikuta katika wakati mgumu mbele ya kocha Zdravko
Logarusic.
Loga alikuwa akimuacha benchi Mombeki, na hata alipoamua
kumuingiza, wakati mwingine alimtoa katika mechi baada ya kufanya kosa kidogo,
jambo ambalo wazi limemkera mshambuliaji huyo mwenye nguvu na ameamua kwenda
kujaribu maisha mapya.
Mombeki alisema kuwa bora aende kutafuta maisha mapya kuliko
kukaa sehemu ambayo atakiwi. “Ndiyo nipo JKT Ruvu sasa, naangalia ustaarabu
mpya,”. Meneja wa JKT Ruvu Suleiman Oga amesema
wamempokea Mombeki na wapo katika mazungumzo naye kwa ajili ya kumsajili.
Pia aliekuwa kocha msaidizi wa kabu ya Yanga na sasa ni Kocha
Mkuu JKT Ruvu Freddy Felix Minziro amesema amempanga Mombeki JKT
Ruvu ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment