Wachezaji zaidi wanatarajiwa kujitokeza kuanzia kesho, huku klabu hiyo ikiendelea na mchakato wa usajili baada ya kutema wachezaji 11 kutoka kikosi cha msimu uliopita na wawili kuondoka.
Yanga imewaacha kipa Yusuph Abdul, mabeki David Luhende, Ibrahim Job, viungo Athuman Idd 'Chuji', Geroge Banda, Rehani Kibingu, Hamisi Thabiti, Bakari Masoud, Abdalllah Mguhi ‘Messi’ na washambuliaji Reliants Lusajo na Shaaban Kondo.
Lakini tayari Yanga imekamilisha usajili wa wawili wa timu ya soka ya taifa ,Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij. Wachezaji waliosajiliwa ni beki Pato Ngonyani, kiungo mkabaji, Said Juma na mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Saleh Abdallah.
Ngonyani anayecheza kushoto na nafasi zote za kati, amesaini Mkataba wa miaka mitatu, wakati Said Juma amesaini miaka miwili na Saleh Abdallah amesaini miaka mitatu pia.
Aidha, Yanga imewaongezea mikataba wachezaji wake Jerry Tegete, Said Bahanuzi, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Ally Mustafa ‘Barthez’ ambao wote wamesaini miaka miwili kila mmoja. Yanga imesitisha mpango wa kumtema kiungo Nizar Khalfan ambaye amebakiza mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment