Thursday, May 15, 2014

VIDEO YA KUPIGWA JAY Z YAUZWA MILIONI 400, MFANYAKAZI ATIMULIWA

Hotel moja jijini New York, nchini Marekani imemfukuza kazi mfanyakazi wake kwa kosa la kusambaza video inayomuonesha Jay akipigwa na Solange ndani ya lifti huku mke wa Jay Z, Beyonce akishangaa bila kufanya lolote.

Video hiyo ambayo imesambaa duniani kwa njia ya mitandao, inamuonesha Jay Z wakiwa ndani ya lift baada ya kuvamiwa na kupigwa hakufanya kitu, bali kujifanya mjinga na kupokea kibano toka kwa shemeji yake ambaye ni mdogo wa mke wake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press nchini Marekani, Hoteli hiyo inayoitwa Standard Hotel, ilimfukuza kazi mfanyakazi wake ambaye alikuwa katika kitengo cha ulinzi kwa “kosa la kutoa taarifa za kipolisi na kurekodi taarifa za siri zilizoonekana katika kamera za CCTC”
Hoteli hiyo pia ilisema kuwa video hiyo iliyorushwa iliwashtua na kuvunjika moyo,na kwamba sasa itawalazimu kutoa maelezo yote kwa polisi.
Mfanyakazi huyo aliuuza video hiyo kwa wamiliki wa mtandao wa TMZ, ambao inasemekana waliinunua kwa dola za kimarekani 250,000 (sawa na shilingi za Tanzania 412,500,000), chanzo kilieleza.
“Jay aliwaambia neno baya Beyonce na Solange na ndo akamrukia. Wakati wakiwa kwenye lift, inaonesha tu jinsi mambo ya ndani ya familia yanavyoweza kubadilika ghafla. Solange anamlinda sana dada yake. “ chanzo hicho kiliongeza.

TAFADHALI SHUKA CHINI UTOE MAONI YAKO. . .


No comments:

Post a Comment