Mkutano Mkuu wa Wanachama wa mabadiliko ya baadhi ya vipengele kwenye katiba utafanyika siku ya jumapili Juni Mosi 2014 katika
ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay kuanzia saa 3 asubuhi
huku wanachama wote hai wa klabu ya Young Africans wakiombwa kujitokeza kwa
wingi .
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu , Afisa
Habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema mkutano huo wa siku ya jumapili ni kwa
ajili
ya marekebisho ya katiba kama maagizo ya Shirikisho la Soka
nchini TFF ilivyoagiza .
Jumapili tunafanya makutano wa marekebisho ya katiba lengo
ni kuhakikisha wanachama wanapata nafasi ya kutoa maoni yao na kupitisha hivyo
vipengele
ambavyo vitapelekea Yanga kupeleka katiba yake TFF na kisha
kwa msajili ili shughuli zote za klabu ziweze kufanyika kwa kufuata katiba mpya
alisema Kizuguto .
Mara baada ya mabadiliko hayo nadhani tutakua tayari
kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi kwani tulikuwa tunasubiria marekebisho ya
Katiba tu, TFF na msajili wakishaipitisha Katiba basi tutakua tayari kuelekea
kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi .
Watakoruhusiwa kuhudhuria mkutano mkuu siku ya jumapili ni
wanachama wa Yanga SC walio hai tu, kwa maana ambao wamelipia ada zao za
uanachama mpaka kufikia kwa mwezi ujao wa Juni 2014 .
Wanachama ambao bado hawajalipia Ada zao za uanachama
wanaombwa kulipia
mapema kabla ya siku ya mkutano , malipo yote yanafayika
kwenye Idara ya Fedha makao makuu ya klabu kila siku muda wa kazi na siku ya
jumamosi saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana .
No comments:
Post a Comment