Wednesday, May 21, 2014

ETI DIAMOND ANAUCHAWI? NAFIKIRI TUNAHITAJI UCHAWI WAKE KWA MAFANIKIO

Diamond Platnumz msanii maarufu Tanzania na sasa tunaweza kudiriki kusema Afrika pia, hiyo ni kutokana na watu wengi kudai anatumia uchawi, lakini kwa jinsi alivyo wafunga tela wasanii mbalimbali kutoka Afrika na kuwaburuza kwa kuzoa kura nyingi katika tuzo zinazo tarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Bw. Platnumz kama jina lake anazidi kung'ara katika anga ya muziki na kuipeperusha bendela ya Tanzania vyema. Mpaka kufikia asubuhi hii Diamond ameshazoa karibu asilimia 70 ya kura zilizopigwa mpaka sasa. Nafikiri kama kuna tunachoweza kufanya ni kuiga anachofanya au hata njia ya mafanikio aliyopita mpaka kufikia hapo.

Simaanishi wote tuwe wasanii, lakini hardworking na commitment kwenye kila tunachofanya. Chini ni matokeo kama yanavyoonekana mpaka tunakwenda mitamboni.





No comments:

Post a Comment