Thursday, May 15, 2014

DIAMOND AZIDI KUPAA KATIKA FANI YA MUZIKI, YUKO BET SASA ANAWANIA TUZO


Msanii wa maarufu wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Diamond Platnumz (pichani Juu) amezidi kuchana anga za muziki duniani kwa kuingia na kutajwa katika kinyang'anyiro cha tuzo muhimu zaidi duniani za BET (Black Entertainment Television) za nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao wa BET, Diamond ameingizwa katika kinyang;ganyiro hicho na kuwania tuzo ya mwanamuziki bora wa kimataifa Afrika, huku nyimbo yake ya "Number One" ndio ikishindanishwa.
Diamond aliandika na kupost katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, akimshukuru mungu kwa kufungua milango kwa muziki wa Tanzania. Katika post hiyo aliyoweka usiku wa kuamkia leo, iliungwa mkono na watu si chini ya 1850, kabla ya asubuhi.
"Dah! am out of words, ….Asante sana Mwenyeso Mungu Baba kwa kwa kuzidi kufungulia milango muziki wetu" Diamond aliandika katika post hiyo. nao mashabiki kadhaa walishindwa kuzuia hisia zao kwa kuunga mkono jitihada zinazofanyika na kumuunga mkono Diamond.
Mamsekwa aliandika"Dah yaani nilivyosoma zile post kuna kina beyonce kina jay z kina nani na nani majina makubwamakubwa ulimwenguni yaani dah hongera sana dangote"
Naye Amrat_96 aliandika "hongera xaaaaaaaaaaaana mkaka bt ucmxahau madam wang wema mi naamn yy ndo anakuxuport xana, bg up!!!!!!"
NA WEWE MSOMAJI SHUKA CHINI UANDIKE MAONI YAKO...





No comments:

Post a Comment