Saturday, May 17, 2014

BREAKING NEWS: MSANII WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA

Fani ya filamu nchini Tanzania imepata pigo kubwa baada ya msanii wa Bongo Movies, nchini Tanzania kufariki dunia jana jioni wakati akielekea kwenye eneo la kupiga picha jijini Dar es Salam. Adam Philip Kuambiana(KULIA) ambaye pia ni mume wa msanii wa music wa kizazi kipya Stara Thomas, alidondoka ghafla akiwa na wasanii wengine ambao ni pamoja Ray.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina anasema walikuwa wanaelekea kwenye kufanya shooting ya sinema mpya ambayo inamhusisha pia msanii maarufu jijini, Ray Kigosi. “Tulipofika maeneo ya Kisutu, Adam alilalamika tumbo linamuuma, hiyvo akaenda kujisaidia na ndipo aliporudi akalalamika kuwa aliharisha sana damu na hajisikii vizuri” kilieleza chanzo hicho.
Inadaiwa wakati Adam anaendelea kulalamika ghafla akaanguka chini na kupoteza fahamu. Wakati wanahangaika kumkimbiza hospitali, akafariki dunia. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali huku msiba unaendelea nyumbani kwa marehemu, Sinza jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment