Wakati Bunge Maalumu la Katiba linaendelea mjini Dodoma,
Mwenyekiti wa Kundi la Wachache, Mh.Freeman Mbowe akitoa maoni ya wachache
mbele ya Mwenyekiti wa Bunge hilo Samweli Sitta, alimtaja Makonda kuwa ni mmoja
wa watu wasioeleweka.
Mbowe alimgeuka Makonda bungeni, akidai kuwa huwa anawauunga
mkono kwa yale ambayo wanafanya ndani ya bunge. Mbowe anadai kuwa wakiulizwa kwanini
wao hawasemi ndani ya bunge, wao hujibu kuwa wanaogopa kushughulikiwa.
Mh. Paulo Makonda aliomba kutoa taarifa, na aliporuhusiwa
alimtaka Mh. Mbowe kumtaja mnafki mmojawapo. Mbowe alisema “nitamtaja mmoja tu, mtu huyo ni Makonda”
kisha akaendelea na hotuba yake.
No comments:
Post a Comment