Tuesday, March 04, 2014

PAPA FRANCIS "ATUKANA" KWENYE MISA TAKATIFU

Wakati anaendesha misa takatifu mjini Vatican, Papa Fancis kwa bahati mbaya alijikuta akitukana na kutumia neno ‘F***’ (likimaanisha Kuto**ba) kwa lugha ua kiitaliano na haraka kurekebisha usemi wake.

Muda mchache baada ya kutamka neno hilo mitandao ya kijamii na tovuti mbalimbali nchini Italy waliweka kosa hilo, ikiwa ni pamoja na mtandao wa YouTube, na hatimaye kusababisha watu wengi kuvutwa ili kujua kilichotokea.

Neno alilotumia Papa ni ‘caso’ likimaanisha ‘maana’ lakini kimakosa alitamka neno ‘cazzo’ likimaanisha ‘f**k’ kwa lugha ya Kiitaliano, hata hivyo wengi ambao hawaelewi lugha hiyo, neno hilo liliwapita bila kuelewa.

SOMA ZAIDI...
 

Papa Francis mwenye umri wa miaka 77 amekuwa mstari wa mbele akisisitiza amani duniani na kutafuta ufumbuzi wa amani kwa njia ya mazunguzo katika mgogoro unaoendelea nchini Ukraine.

Akihutubia kutokea kwenye dirisha la jengo(PICHANI JUU) analoishi jijini Vatican, alisema “ ni matumaini yangu kwamba kila kila anayehusika nchi humo atafanikiwa kupambana na kujenga taifa la baadae. Kwa moyo mmoja naiomba jumuiya ya kimataifa kuunga mkono kila jitiada za kuleta amani.

“Moyo wenye kutamani kumiliki ni moyo usio na uungu. Kwa maana hii, Yesu mara nyingi aliwaonya matajiri kwa sababu wako kwenye nafasi kubwa zaidi ya kulinda utajiri wao zaidi hapa duniani”

Katika “f****g” kwa maana hii majaliwa ya mungu yanaonekana kama ni mshikamano”

Pamoja na kukosea huko, Papa Francis aliendelea vizuri tu na kurekebisha usemi wake haraka, wakati umati ukiwa umekusanyika katika viwanja vya St Peter na wale wanaoangalia na kusikiliza katika maeneo mbalimbali duniani walijiuliza “hivi amesema F**k?”

Kwenye mitandao ya kijami, kuteleza huko kulisababisha watu wengi sana kurudi na kufuatilia kutaka kujua nini kimetokea, lakini wengi pia walidai ni kosa la kibnadamu na kwamba hakufanya makusudi, lakini wako waliotafsiri kuwa hilo ndilo linalothibitisha kuwa Papa huyo ni “mtu wa watu”

Msemaji wa Vatican hakutaka kuliongelea hilo.







No comments:

Post a Comment