Ni muda mfupi tu toka Uganda ipitishe sharia ya kupinga
ushoga, imeripotiwa mtu mmoja aliyetuhumiwa kuwa shoga alichomwa moto mpaka
kufa nchini humo.
CNN imeripoti tukio hilo ambalo jina la mtu (KULIA PICHANI) huyo
halikuweza kujulikana. Picha ilionesha jinsi mtu huyo anavyochomwa moto huku
akiwa pembeni mwa reli huku watoto wakishuhudia tukio hilo.
Sharia hiyo iliyopitishwa hivi karibuni, inahusisha
pamoja na kufungwa maisha kwa mtu yoyote atakayejihusisha na shughuli zozote za
ushoga pamoja na kuambukiza ukimwi, matendo ya ngono na watoto pamoja na watu
wenye ulemavu, udhalilishaji ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Sharia hiyo iliyozaliwa mwaka 2009, na kupewa jina “Kill
The Gays” ikimaanisha “Ua Mashoga” ambayo ilisisitiza hukumu ya kifo kwa
matendo fulani ya ushoga, lakini ilirudishwa kabatini kutokana na kelele nyingi
zilizopigwa na mataifa mbalimbali.
Katika sharia hii mpya, mtu yeyote atakaye fungisha ndoa
ya jinsia moja atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 7. Atakayeshindwa kutoa
taarifa ya ushoga polisi pia ni mualifu.
Madaktari watakao watibu mashoga, watakaopangisha mashoga
kwenye nyumba zao na wale wataka shukiwa kuwa mashoga, wasagaji, waliobadilisha
jinsia na mabasha watafungwa miaka 5.
Mtu yeyote atakayetoa msaidia kwa shoga atakuwa anavunja
sharia, ambapo atachukuliwa hatua.
Watu wengi wanaamini kuwa sharia hii ni muhimu ili
kupinga tabia na tamaduni za nchi za magharibi. “ hii sharia ni muhimu kwa nchi
hii ili kulinda tamaduni za Mwafrika” alisema David Bahati ambaye ni mbunge
ambaye aliuwakilisha muswada huo bungeni.
Bahati pia ni mmoja kati ya kundi linalotuma fedha katika
nchi za Afrika kuunga mkono wanaopinga shughuli zote za ushoga.
No comments:
Post a Comment