Tunduru,
Kijana wa miaka 18 mkqazi wa Kijiji cha nakapanya Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Abdalah Yusuph amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya hiyo kujibu tuhuma za kumbaka mama mwenye ulemavu.
Kwa mujibu wa taarifa za tukio hilo mtuhumiwa huyo alifanikisha kutekeleza adhima yake hiyo baada ya kumtishi kwa kumchoma kisu endapo angemzuwia kufanya tendo hilo kwa njia yoyote ile ikiwemo kupiga makelele ya kuomba msaada kwa watu.
Akimsomea shtaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Charles Mrema, mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa polisi Inspekta Songelaeli Jwagu alisema kuwa mtuhumiwa huyo kwa makusudi alitekeleza unyama huo February 27 mwaka huu.
Inspekita Jwagu aliendelea kufafanua kuwa katika tukio hilo mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha vifungu vya sharia namba 131 kifungu kidogo cha (1) na (2) na namba 131 vya sharia ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema katika Tukio hilo Kijana huyo kwa kukusudia slienda nyumbani kwake na kumvamia na kumbaka mlemevu huyo wa mguu na mkono aliyefahamika kwa jina la Somoye Abdalah (48) baada kuvamiwa majira ya saa 1 za usiku wa siku ya tukio hilo.
Mtuhumiwa huyo alikana kufanya kosa hilo, amepelekwa mahabusu ya gereza la Wilaya ya tunduru baada ya kukosa mtu wa kumdhamini, Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika kesi italekwa tena march 17 mwaka huu katika mahakama hiyo kwa ajili ya kutanjwa .
No comments:
Post a Comment