Sunday, March 30, 2014

AJALI YAKUTISHA: YAUA WANAWAKE 12, WAKIELEKEA MSIBANI (SOMA MAJINA YAO)


File photo Same.
Same.

Watu 12 wamefariki dunia, 10 papo hapo, baada ya ajali mbaya iliyotokea eneo la Hedaru, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro na kuhusisha magari matatu.

Akidhibitisha jana kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema ajali hiyo ilitokea juzi usiku saa mbili na kwamba mtu mmoja  alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya KCMC, iliyoko Moshi.

"Ajali hii iliyahusisha magari matatu ambapo gari lenye usaji nambari T 299 ANM aina ya Fuso lori lililokuwa likitokea Moshi kuelekea Dar es Salaam, likiendeshwa na dereva ambae jina lake halijafahamika, liligonga nyuma gari Toyota Hilux ( T 170 AKZ)  lililotokea Hedaru kwenda Majengo Moshi", alisema na kuongeza dereva wa gari liligongwa ni Gerard Mgwe ambaye ni diwani wa Kata ya Hedaru.

ENDELA KUSOMA . . .


Alisema baada ya gari, Hilux kugongwa nyuma na lenyewe likagonga kwa mbele gari aina ya Scania (T 737 AKW) na Tela (T 776 CCN) lililotokea Dar es Salaam kuelekea Moshi na kusababisha vifo vya watu wote 12 ambao ni wanawake waliokuwa wakiekea kwenye msiba wa mtoto ambaye aliefariki kwa kusombwa na maji yaliyosababishwa na mvua akubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Aliwataja waliofariki ambao wote ni wakulima na wakazi wa Kongei Hedaru kuwa ni Stella John (45), Salma Kizoko(33), Mary Senzighe(49), Neema Daniel(52), Rehema George(29) na Sofia Mbike(51).

Wengine ni  Mama Rita Kalani(55), Mama Kalani Stephano(55), Kolina Mmasa(55), Bahati Daudi(25), Farida Kiondo(24) na Maria John(33). Wengine 7 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kwamba 3 kati yao wako katika hali mbaya wakiwa wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Zubeda Mrindoko(42), Mipa Chedieli(29) na Zubeda Mlita(32 ), wote ni wakazi wa Kongei Hedaru.

Kamanda Boaz aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Joyce Kandogwe(29), Subira Juma(22) wote wakazi wa Kongei; Ramadhan Msangi, (31) na Adinan Rajabu, wote ni madereva wakazi wa Moshi. Miili yote imehifadhiwa katika hospitali ya Same na kwamba jitahada za kumtafauta dereva aliesababisha ajali zinaendelea.


No comments:

Post a Comment