Thursday, January 16, 2014

WAVAMIA KITUO CHA POLISI KUSHINIKIZA, MWENZAO AUAWA

Tabora

Mtu mmoja ameuawa na mwingine kujeruhiwa kufuatia wananchi wenye hasira kuamua kuvamia Kituo kidogo cha Polisi kwa lengo la kumtoa mtuhumiwa kwa lengo la kumuua.
Picha kwa hisani ya mtandao
Tukio hilo limetokea baada ya wananchi wa Kijiji cha King'wangoko, Kata ya Sasu wilayani Kaliua kuvamia Kituo kidogo cha polisi ili kumdhurU Shija Matenga, anayetuhumiwa kwa kosa la wizi wa ng'ombe watano.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Peter Ouma, alisema Mkuu wa kituo Kidogo cha King'wangoko, alipokea simu kutoka kwa wakala wa mnada wa Konanne kuwa wananchi wamemkamata mwizi na kumfunga kamba na wanataka kumuua.

Alieleza kuwa mkuu wa kituo hicho alituma askari wawili wakiwa na silaha na kumuokoa mtuhumiwa na kuanza kuondoka naye kitendo kilichokasirikiwa na wananchi ambao walianza kurusha mawe na fimbo ili kuwazuia askari wasimpeleke kituoni kitendo kilichosababisha askari kupiga risasi hewani ili kuwatawanya wananchi.


Kwa mujibu wa kamanda Ouma baada ya askari hao kumfikisha mtuhumiwa kituoni na kumfungia mahabusu, wananchi walimfuatilia mtuhumiwa huyo kituoni hapo na kushinikiza atolewe ili wamdhuru.

Aliongeza kuwa askari walipoona wananchi wanataka kutumia nguvu walifyatua risasi hewani ili kuwatawanya na risasi moja ilimpata John Joseph katika bega la kulia na kufariki papo hapo.

Mtu mwingine aitwaye Malembeka Matemele alijeruhiwa kwa risasi katika paja la kulia na amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Urambo

Kamanda Ouma aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa watuhumiwa kwani ni kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment