Thursday, January 16, 2014

MAAJABU YA ELIMU FINLAND, ANGALIA JINSI TUNAVYO TOFAUTIANA

Shule za Finland wanafunzi hawavai sare (kama za kwetu, kwanza kwetu ni sharia kabisa kuvaa uniform), hakuna mtihani wa majaribio (interview) ili kuanza shule, hakuna ada ya kiingilio, hakuna kushindana nani kafanya vizuri nani vibaya, hakuna ukaguzi wa kushtukiza mashuleni (kujenga mazingira ya kitu kidogo zaidi ya hali halisi).

Kama haitoshi, sikia hii hapa sasa: hakuna mtoto kuanza shule kabla ya kufikisha miaka 7 (bongo wanaanza wakiwa na miaka 3 mpaka 4, kwa madai wana akili sana), watoto hawapangwi kwa uwezo, eti labda wenye akili kuliko wengine darasa tofauti, kwanza ni kinyume cha sharia( kwetu kuna shule maalumu za wenye akili kuliko wengine – hivi wale wanaishiaga wapi?).

Watoto wanawaita walimu wao kwa majina la kwanza (Tanzania thubutu ndo utakiona cha mtema kuni), na wanafunzi hawapewi homework watakazofanya zaidi ya nusu saa wakiwa nyumbani (hapa nafikiri tunawazidi, maana hakuna kabisa homework labda shule za private).

Cha ajabu sasa: tokea mwaka 2000, Finlad ni kati ya nchi duniani zinazoshika nafasi ya kwanza katika kiwango cha elimu duniani (Tanzania sijui ni ya ngapi).

Tanzania tunajifunza nini hapa..!



No comments:

Post a Comment