Thursday, January 23, 2014

KLABU TAJIRI KULIKO ZOTE DUNIANI KWA ZAIDI YA MIAKA 9


Wachezaji wa Real Madrid
Klabu ya Real Madrid imehifadhi taji la kuwa klabu tajiri zaidi duniani kwa msimu wa tisa mfululizo, kuambatana na orodha ya vilabu tajiri iliyochapishwa na kampuni ya uhasibu ya Deloitte.

Klabu nyingine ya Uhispania, Barcelona inashilikia nafasi ya pili ikifuatwa na Bayern Munich ya Ujerumani, katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.

Kwa mara ya kwanza klabu ya Manchester United ambayo kwa sasa imekabiliwa na msururu wa matokea mabaya katika ligi kuu ya Premier ya England, imeshushwa miongoni mwa vilabu tatu tajiri zaidi duniani kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na saba iliyopita.

Waandishi wa habari wanasema kuwa ligi ya vilabu vingi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha, nyingi ya vilabu hivyo vinaendelea kupata hasara kubwa kutokana na gharama za mishahara na malipo ya usajili wa wachezaji.(BBC)


No comments:

Post a Comment