Monday, December 23, 2013

MAJANGA: KUMBE WANAUME PIA WANABAKWA!!

ATEKWA, ATISHIWA KISU, KISHA ABAKWA BILA KINGA 

Mwandishi Wetu

Polisi inadaiwa kuchunguza tuhuma nzito ya uvamizi na ubakaji usio wa kawaida kwa kijana wa miaka 30 linalodaiwa kutokea hivi karibuni ambapo wanawake wawili wanadaiwa kuhusika.
Tukio hilo lililotokea ijumaa iliyopita linadaiwa kuwa ni moja ya matukio hatari ambayo yamekuwa yakitokea nchini, na kuwaacha polisi kutojua la kufanya.
Muathirika mmoja wapo, kwa mujibu wa polisi ni mtembea kwa miguu mmoja ambaye alikuwa anaelekea jijini Harare na kulazimika kuomba lifti akiwa katika kituo cha mafuta cha AMTEC karibu na barabara ya Lobengula, jijini.
Ilikuwa ni baada ya saa 3 jioni, tarehe 29 aprili, muhusika alifuatwa na mwanamke aliyemuelezea kuwa na umri unaokisiwa kuwa miaka 40 ambaye alimwambia katika maongezi yao kuwa nay eye anaelekea Harare.
Baadae kidogo, polisi wanasema gari aina ya Toyota Cauding iliyokuwa inaendeshwa na mwanamke na abiria wa mwanaume akiwa amekaa nyuma ilisimama.
“dereva akasema anauwezo wa kubeba abiria wengine wawili tu kuelekea Harare. Mlalamikaji akaingia nyuma na mwanamke akaingia kiti cha mbele” alidai msemaji wa polisi Inspector Patrick Chademana.
Polisi wanadai kuwa kilometa chache baadae nje ya Gweru, dereva aliwasha endiketa na kupunguza mwendo kuashiria kusihiwa mafuta na kuingia kituo cha mafuta cha Consilla.
“ghafla, mwanaume aliyekaa kiti cha nyuma na mlalamikaji akatoa kitambaa kinachodaiwa kuwa na dawa ya usingizi na kumziba mlalamikaji mdomo na pua na kisha upoteza fahamu” inspekta Chademana aliongeza
alipozinduka alijikuta ndani ya chumba chenye zulia la rangi ya brown na sofa la ngozi. Mwanaume aliyekuwa abiria akiwa ameshika kisu, polisi walieleza.
“mlalamikaji wanawake wale wawili walivua nguo zote na kubakia uchi wa mnyama na kumfuata. Akalazimishwa kufanya ngono zembe na wanawake hao wawili huku akiwa ameshikiwa kisu,” alisema Chademana.
Baada ya shambulio hilo, polisi wanadai mlalamikaji alizibwa tena mdomo na dawa mpaka akapoteza fahamu na alipozinduka mapema jumamosi asubuhi alijikuta katika pori karibu na kona ya St.Patrick karibu na njia kuu ya kuelekea Harare kutoka Gweru.

Pamoja na tukio hilo pia alporwa pesa zote, simu yake ya mkononi, na mali alizokuwa nazo zenye thamani isiyopungua laki mbili na nusu.

Chademana aliongeza: “tuna toa rai kwa watu wote wenye kujua lolote kuhusiana na watuhumiwa hao atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi kilicho karibu”
“pia tunatoa taadhari kwa wasafiri wote kuacha kuingia kwenye magari wasiyoyatambua ili kupunguza uwezekano wa matukio ya ubakaji”




No comments:

Post a Comment