MSANII maarufu zaidi nchini, Diamond Platnum, ametangaza jana kufanya tamasha kubwa na la kihistoria kwa watoto katika viwanja vya Leaders tarehe 25 ya mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Diamond alisema lengo kuu la tamasha hilo ni kuonyesha upendo wake kwa watoto lakini pia kuwashukuru kwa kumuunga mkono kwa kipindi chote cha uimbaji wake.
‘’Nimekuwa na bahati kwa muziki wangu kupendwa na watu wa rika zote, na kwa bahati nzuri wa marika mengine wamekuwa na bahati ya kuhudhuria matamasha yangu tofauti, ambayo watoto hawawezi kufika na ndio maana nikaona nao kuna haja niwafanyie kitu cha peke yao”alisema Diamond.’
Diamond ambaye kwa wiki mbili zilizopita amekuwa akizunguka kwenye vituo tofauti vya watoto yatima kuwapa misaada mbalimbali, anasema tamasha hilo ambalo itakuwa la mara ya kwanza kwa msanii mkubwa kufanya tamasha na watoto litaweka historia nchini.
Aliongeza kuwa anataka kuwapa watoto nafasi ya kuifurahia siku hiyo kwa kuwaandalia michezo mbalimbali, burudani maalum kutoka kwake, pamoja na nafasi ya kuzungumza nao mambo mbalimbali.
Pia, tamasha hilo ambalo litaanza saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni,litawapa fursa watoto kumsikia Diamond akiwaeleza kuhusu maisha na namna wanavyoweza kuamini ndoto zao na kufikia malengo yao ya kimaisha.
‘’Naamini mimi ni mfano kwa watoto wengi ambao ni role model , na hivyo pia nitatumia nfasi hiyo kuwapa moyo kukazana kuhakikisha wanazifikia ndoto zao”,alisisitiza Diamond.
Naye Mratibu wa tamasha hilo, Babu Tale, alisema maandalizi ya tamasha mpaka sasa yanaenda vizuri na hivyo watoto wajitokeze kwa wingi siku hiyo.
Alisema michezo mbalimbali ya watoto itakuwepo siku hiyo lakini pia kutakuwa na zawadi mbalimbali zitatolewa kwa watoto watakaoonyesha vipaji vya kipekee.

No comments:
Post a Comment