Tuesday, August 13, 2013

HII KALI: DAKTARI AIBA HEROINE TUMBONI MWA MGONJWA


Polisi nchini Urusi wamemzuilia daktari mmoja mpasuaji kwa madai ya kuiba kifuko kilichokuwa na dawa ya kulevya ya Heroin kutoka tumboni mwa mgonjwa.

Polisi katika eneo la Siberian walimtaka daktari kumfanyia upasuaji mshukiwa ili waweze kunasa dawa hiyo ambayo mgonjwa alikuwa ameimeza. Hata hivyo polisi waligundua kuwa seheme ya dawa hiyo iliyotolewa tumboni mwa mshukiwa ilikuwa inakosekana

Maafisa wa utawala wanadai kuwa daktari huyo alikuwa amelewa walipomkamata.

Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, iwapo atapatikana na kosa la kuiba dawa za kulevya atahukumiwa kifungo cha miaka 15.


No comments:

Post a Comment