Tuesday, July 02, 2013

YALIYOJILI TUZO ZA BET 2013, ICE PRINCE AWABWAGA AKINA 2FACE


MUIMBAJI wa Nigeria, Ice Prince amewabwaga wasanii wenzake wa Afrika akiwemo 2Face Idibia (Nigeria), Toya Delazy (Afrika Kusini), R2Bees (Ghana), na Radio Weasel (Uganda), baada ya kuibuka kidedea katika kipengele cha 'Best International Act Africa' katika  tuzo za BET zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Marekani.

Ice alionekana kuwabwaga wasanii hao kutoka Afrika kwa kuinyakua tuzo hiyo, ambayo aliamini imetokana na juhudi zake.


Tuzo hizo ambazo zilihudhuriwa na nyota mbalimbali akiwemo Radio na Weasel, ambao waliweka wazi kuwa hata kama wakikosa tuzo hizo kitendo cha wao kutajwa kwenye kipengele hicho ni heshima kubwa kwa kutambulika kutokana na kazi yao.

Wakati huo huo, Miguel aliyenyakua tuzo ya muimbaji bora wa kiume wa 'R&B na pop', ambaye yeye aliwagalagaza Brown, Timberlake, Usher na Bruno Mars.

Baada ya kupata tuzo hiyo, Miguel aliamua kuutumia usiku huo kumkumbuka Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela; "Tunataka kuchukua muda na kutuma salamu na fikra zetu kwa mtu aliyeubadilisha ulimwengu," alisema.

Tuzo hizo ambazo zilipambwa na shoo mbalimbali ambapo, Chris Brown ndiye aliyefungua shoo kwa kutumbuiza nyimbo ambapo, Nick Minaj aliungana naye jukwaani hapo kwa ajili ya kutumbuiza nyimbo walioshirikiana.

Tuzo za BET, zinafanyika kila mwaka kwa ajili ya kutoa tuzo kwa wasanii waliofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka mzima, ambapo tuzo hizo mwaka huu zilifanyika jijini Los Angeles Marekani.



 Muimbaji Brand akiwa amepozi ndani ya red carpet kabla ya kuingia ukumbini hapo kushuhudia tuzo hizo
 Jamie Fox sambamba na Ciara wakifanya shoo usiku wa tuzo hizo
 Ice Prince aibuka kidedea tuzo za BET

 Hii ilikuwa ni moja ya burudani ambazo zilitolewa usiku huo



No comments:

Post a Comment