Thursday, July 18, 2013

GILLIE KUIGIZA FILAMU YA TUPAC



Mfalme wa Philly maarufu kama Gillie Da Kid anatarajiwa akishirikiana na wakongwe wa filamu Ving Rhames na Steven Seagal katika filamu itakayoitwa “Force of Execution,” huku akiendelea kupigia debe filamu ya Wrath of Cain, King of the Avenue na Mafia.

Gillie pia najaipanga kucheza kama staring kwenye filamu mpya ya Suge Knight. Katika filamu hiyo, msanii huyo rapa wa Philladelphia nchini Marekani atacheza kama Tupac Shakur.


“Ni dhahiri kwamba tunayo bajet tayari, hivyo nasubir kujua ni lini tunaanza kurekodi” Gillie aliuambia mtandao mmoja maarufu wa AllHiphop.com, “mimi sio mwongozaji katika filamu hiyo bali ni mcheza filamu tu. Nikiambiwa muda wa kuchapa kazi umefika, naingia kazini, kila kitu kipo tayari” alisema Gillie

Gil Smith maarufu kama Gillie hakujizuia kuonyesa msisimko kumbwa akitaka kuonesha uwezo wake wa kucheza sinema katika filamu hiyo inayokuja.

“we jua tu kwamba nnakwenda kubadilisha mambo kama Will Smith alivyocheza filamu ya Ali” alidai Gillie “ tunajua mimi ni mzuri kiasi gani kucheza kama Pac, hapo hakuna swali haswa wakishaniwekea makeup kidogo tu, nimeingia gym najaribu kuongeza uzito kidogo tu kufikia kufanana na maumbile yake”


No comments:

Post a Comment