Friday, July 12, 2013

ELTON JOHN AUGUA KIDOLE TUMBO


Gwiji wa muziki wa Pop nchini Uingereza, Sir Elton John amelazimika kuahirisha onesho lake lililokuwa lifanyike Hyde Park jijini London, baada ya kubainika kuwa ana tatizo la kidole tumbo.

Nyota huyo wa pop alikuwa atumbuize usiku wa leo, katika onesho ambalo angewashirikisha nyota wengine kama Elvis Costellon na 'The Kinks'


Sir Elton alikwenda kumwona daktari baada ya kurejea akiwa mgonjwa katika ziara yake ya Ulaya, nyota huyo wenye umri wa miaka 66, alifanyiwa uchunguzi mbalimbali hospitalini pamoja na kuchukuliwa vipimo vya damu na sasa anatumia dawa kabla ya kufanyiwa operesheni




No comments:

Post a Comment