Thursday, June 13, 2013

KALA JEREMIAH AANZA SAFARI KUPELEKA TUZO KWA MAMA NGWEA

Msanii wa kizazi kipya ambaye ndio msanii bora wa muziki wa Hip Hop katika tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2013, Kala Jeremiah akiwa na kundi la marafiki zake asubui hii kuelekea Morogoro kukabidhi tuzo hiyo kwa familia ya marehemu Albert Mangwea.


Pamoja na kupekea tuzo hiyo, akiieleza blog ya Imma Matukio, Kala alisema 'naamini kuwa Ngwea ndie msanii bora zaidi katika music wa Hip Hop kutokana na mchango wake katika tasnia hii'. 
Kala Jeremiah alichaguliwa kushindania tuzo 4, katika tuzo hizo kubwa na maarufu kuliko zote nchini Tanzania zinazodhaminiwa na kampuni ya Tanzania Breweries Limited kila mwaka ambapo alizoa nafasi 3.
Nafasi alizoshinda ni nyimbo bora ya hip hop, msanii bora wa hip hop pamoja na mtunzi bora wa hip hop.

Kala Jeremiah akiwa na kundi lake ameanza safari kuelekea Morogoro kupeleka tuzo kama alivyoahidi. Katika msafara huo anaambatana na washkaji zake katika safari hiyo. Immamatukio itaendelea kukujuza msafara mzima ikiwa ni pamoja na picha za matukio mbalimbali katika shughuli hiyo.
Don't touch that dial


No comments:

Post a Comment