Sunday, June 30, 2013

BARACK OBAMA AELEZA KWANINI HAENDI KENYA



Alikuwa anajibu swali aliloulizwa na Wakenya, kuhusu ahadi ya kutembela nchi ya Kenya mahali alipozaliwa baba yake mzazi katika kipindi chake cha urais. Alikuwa anaongea na mamia ya vijana waliokutana nae Soweto, Chuo Kikuu cha Johannesburg leo.

“Bado ntakuwa Rais kwa miaka mingine mitatu na nusu” alijibu alipoulizwa kwa kutumia video ya kwenye mtandao kutoka Nairobi kwanini hatotembelea  Kenya.



“Unagundua kama Rais watu sio tu wanataka utekeleza ahadi zako lakini wanataka utekeleze ahadi zao jana” alisema Obama alipokuwa anajibu swali hilo.

Lakini Obama alikubali kwamba maamuzi ya mahakama ya kimataifa ya ICC yamechangia maamuzi yake ya kutokwenda Kenya

“Sidhani kama ulikuwa wakati muafaka mimi kutembelea nchi hiyo” alisema huku akiendelea kusisitiza kwamba bado ana mpango wa kwenda Kenya kabla muda wake wa urais haujaisha, ambapo itakuwa mwaka 2017

Mapema katika mkutano na vyombo vya habari akiwa mjini Pretoria, alisema kuwa ameiruka Kenya katika ziara yake kutokana na migogoro, ambapo ICC inamshtaki Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa makosa ya uhaini, yanayo husu mauaji, ubakaji, unyanyasaji na unyama ambayo yaliyofanywa na wafuasi wake katika fujo za uchaguzi wa Kenya wa mwaka 2007. 

“Muda sio muafaka kwangu kama Rais wa Marekani kutembelea nchi ya Kenya wakati ambao hayo masuala yanaendelea kufanyiwa kazi, na nnategemea yatapatiwa ufumbuzi

No comments:

Post a Comment