Saturday, April 27, 2013

MTAMBUE FID Q NJE YA MUZIKI



"KUWASAIDIA watoto yatima ndio moja ya kazi inayonifanya kuwa karibu na jamii yangu kwani nao wanahitaji upendo na kujiona kuwa ni moja ya familia kwa kupata misingi na misimamo ya kimaisha" hayo ni maneno yaliyosemwa na muimbaji wa Hip Hop Tanzania Farid Kubanga maarufu kwa jina la Fid Q alipokutana na mwandishi wa habari hii  wiki hii


1. Mbali na kuwa muimbaji wa nyimbo za Hip Hop pia ni mwalimu anayefundisha Ujamaa Hip Hop darasa kwa watoto wa mitaani ili kuwajenga uwezo na kuwasaidia kutimiza malengo yao

2. Ameamua kuanzisha darasa ambapo wanafunzi wake ni watoto wa mitaani wanaoosha magari barabarani ili kuwajengea uwezo na kuwatoa katika hali ya upweke

3.Fid Q ameamua kujikita kuwasaidia watoto wa mitaani kupitia darasa hilo ili kuwajengea fikra mbadala na huku akiwapa mbinu mpya ya kuwakomboa na kuwasaidia kufikisha malengo yao kwa kupitia darasa hilo

4. Anatumia kipaji chake kwa ajili ya kufundisha watoto hao kupitia muziki wa Hip Hop ingawa pia amewatafutia mwalimu wa kingereza ili waweze kujiendeleza na kujua lugha hiyo ya kigeni

5. Fid Q ambaye anaamini kwa kupitia darasa lake atatoa vijana wenye mitazamo tofauti yenye tija kwa jamii yake hivyo kwa kujifunza lugha ya kingereza pia ni moja ya kuwaongezea mwanga wa kuendelea kung'amua mambo mbalimbali

6. Kwa kipindi hiki wapo katika likizo ambapo baada ya kumaliza likizo hiyo wanafunzi hao watakgawanyika katika madarasa manne tofauti tofauti kulingana na mambo wanayoyasoma kwani kila mwanafunzi anasomo lake analojifunza

7. Mbali na kujifunza fikra mbadala pia wanajifunza kuimba pamoja na kucheza kutokana  na uwezo anaowajengea anaamini kuwa atatoa vijana wenye vipaji bora na waliojaa ubunifu wa hali ya juu

8. Anapenda kukaa na watoto wa mitaani kila wakati ili kuwatia moyo na nguvu ili wajione wanaumuhimu mkubwa kwenye jamii yao hususani katika sekta ya kimaendeleo

9. Fid Q ambaye pia ni msanii wa Hip Hop ambaye ameanza kusikika katika sekta ya muziki mwaka 97  ambapo ameshaachia albamu zake mbili na kwa sasa yupo mbioni kuandaa albamu ya tatu huku akiwa na malengo ya kuufikisha muziki wa Hip Hop mbali katika soko la kimataifa

No comments:

Post a Comment