Tuesday, April 16, 2013

ALICHOKIANDIKA LEO ZITTO KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK



Kwanini Wabunge nje ya Kamera wana mahusiano mazuri lakini kwenye kamera wanatukanana? Hili ni swali January Y. Makamba kauli za leo Bungeni. Kwa siku kadhaa tumeshuhudia wabunge wakirushiana maneno ya kifedhuli sana lakini nje ya Bunge wanaitana 'mambo vipi kaka' 'sema ndugu yangu' nk. Jibu ni rahisi sana. Kwanza, Siasa za Tanzania zimejengwa kwenye misingi ya UNAFIKI. Ushabiki huzaa unafiki, hivyo watu wanapotaka shabikia kitu hujikuta wanafanya unafiki ili kuonekana wao ni mashabiki zaidi. Pili, kuna siasa za kujipendekeza kwa wakubwa ili wakubwa waone kuwa 'duh huyu jembe huyu, anatetea sana msimamo wa chama'. Binaadamu wengine wameumbwa hivyo na hivyo ni lazima kukubaliana na hali hiyo na kisha kuweka mikakati ya ku 'manage' hali hiyo. Tufanyeje? @Filikunjombe kasema 'CCM ijikite kwenye kutimiza ahadi zake kwa wananchi ili wapinzani wakose cha kusema' inaweza kuwa hatua mojawapo. Lakini kwa vyovyote CHADEMA hatutakosa cha kusema kwani kuna mambo mengi sana ya kusimamia ili kuhakikisha kuwa wananchi wanafaidi kodi yao.

Suluhisho la kudumu ni kujenga vikundi vya kibunge vilivyo juu ya vyama vya siasa na vyenye maslahi kwa Umma. Kwa mfano mpango wa kuanzisha 'Oil and Gas Parliamentary Caucus' unapaswa kuharakishwa ili wabunge wawe na masuala ya kufanyia kazi na kuzungumza katika nyakati za ku 'socialise'. 'Parliamentary Education Caucus' nayo hivi sasa ni kama inachungulia kaburi. Wabunge wapenda soka na wapenzi wa Taifa Stars tuna kundi la Parliamentarians for TaifaStars, makundi kama haya yanapaswa kudumishwa ili kuwaweka Wabunge katika mahusiano ya kitaaluma badala ya mahusiano ya kunywa na kucheza disco tu. Mahusiano ya Wabunge ya kitaaluma yatamaliza malumbano ya hovyo bungeni na kuruhusu wabunge kuwa na muda wa kutosha kujadiliana kwa hoja na kuisimamia Serikali iwajibike.

Tatizo kubwa Tanzania ni Uwajibikaji. Uwajibikaji ndio suluhisho la UFISADI nchini. Uwajibikaji utapelekea utajiri wa nchi kutumika kuondoa umasikini.Uwajibikaji utaondoa malumbano ya hovyo hovyo Bungeni.
Like ·  · about an hour ago · 
  • 158 people like this.
  • Abduly Mohamed I Agree to Disagree with you Bruv. Kama bado sheria inasema ukipoteza uanachama umepoteza na Ubunge, Ni ngumu kutengenisha Mbunge na Chama. Nje ya Bunge kila mbunge anajua hadha na ukali wa maisha ambayo wananchi wanakabiliana nayo,Lakini ni ngumu kusi...See More
    Like · 2 · 47 minutes ago
  • Gfamily Kagutta Tatizo kubwa Tanzania ni Uwajibikaji. Uwajibikaji ndio suluhisho la UFISADI nchini. Uwajibikaji utapelekea utajiri wa nchi kutumika kuondoa umasikini.Uwajibikaji utaondoa malumbano ya hovyo hovyo Bungeni.Mh.ZITTO KABWE" Hili mh neno! nakubaliana na wewe 100%
    Like · 1 · 33 minutes ago
  • Hellen Lutainulwa too much acting. thr r no permanent enemies in politics thats why politics wl remain to b the dirty game.
  • Haji Lukamba Ni sanaa Zitto Kabwe hujajua kama raia tunachezewa shere


No comments:

Post a Comment