MSANII mahiri katika miondoko ya muziki wa Bongo Flava Barnara, anataraia kuondoka nchini Machi 28, mwaka huu kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya kurekodi kibao chake kipya kiitwacho 'Tuachane kwa Wema, ambacho atamshirikisha mwanamuziki nyota wa muziki wa Dansi Fally Ipupa.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Barnaba, alisema kuwa maandalizi yote ya safari hiyo tayari yamekamilika na tayari amekwishapewa 'Apointment' na moja ya Studio za nchini humo tarehe ya kufika na kurekodi wimbo wake huo. Aidha Barnaba alisema kuwa wimbo huo utakuwa ni miongoni mwa nyimbo zake zitakazokuwamo katika albam yake mpya itakayokuwa na jumla ya nyimbo 10, ambayo inatarajia kukamilika mwezi wa sita mwaka huu.
''Unajua katika ndoto zangu za kimuziki nimekuwa na ndoto siku nyingi ya kurekodi na mastaa wa ukweli Duniani, na Fally ni mwanzo tu kwani wapo wengine ambao tayari nimeshawasiliana nao pande za mamtoni ambao tayarikama watatu wamekwisha nithitishia kunipa 'shavu' katika miongoni mwa nyimbo zangu kadhaa ambazo nyingine zitakuwa ni katika albam yangu ijayo baada ya hii.
Hata Fally pia alikuwa akitamani kurekodi na mimi tangu nilipo mpagawisha katika moja ya shoo yake alipokuja nchini na kuipenda sauti yangu, kwa hiyo naye nipi ni nafasi yake pekee aliyokuwa akiitamani ambayo amefanikiwa'' alisema Barnaba Barnaba alisema kuwa mbali na wimbo huo lakini pia anatarajia kurekodi video ya wimbo huo, awapo nchini humo iwapo atafanikiwa kumaliza ndani ya muda uliopangwa na mwandaaji wake.
Alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwa katika albam hiyo kuwa ni pamoja na Gubegube, Sidhani Kama na Roho si Moyo, ambazo zote tayari zimekwisharekodiwa katika Studio za THT.
na sufianimafoto.blogspot
No comments:
Post a Comment