Eneo la Kitongoji cha Mferejini lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuanzisha kambi kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko .
Wahanga wa Mafuriko wakianza ujenzi wa nyumba za Miti kwa ajili ya kujisitiri katika eneo la Ruvu Mferejini. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
SERIKALI imetoa siku mbili kwa wananchi waliosalia katika Vijiji vya Ruvu Mferejini na Ruvu Marwa wilayani Same ,Mkoani Kilimanjaro vilivyozingirwa na maji kuondoka mara moja na kwamba watakao kaidi wataondolewa kwa kutumia nguvu na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Zaidi ya watu wapatao 2000 wamelazimika kuyahama makazi yao baada ya kufikwa mafuriko kutokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha huku eneo lililoathirika zaidi na mvua hizo ni ukanda wa tambarare wa wilaya ya Same unaopakana na Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Licha ya Idadi hiyo ya watu kuyahama makazi yao lakini bado wapo waliokaidi kuondokana na hapa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Same ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya hiyo ,Rosemerry Senyamule ,ikatoa agizo.


