MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) umesema watatumia maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Jijini Tanga kuwahamasisha wafanyabiashara kujiunga nao ili waweze kunifaika na huduma za matibabu pindi wanakuwa wakikumbana na magonjwa mbalimbali.
Hayo yalisemwa jana na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kwenye ufunguzi wa maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa yanayofanyika eneo la Mwahako mjini hapa.
Alisema watakapojiunga nao wataweza kuwa na uhakika wa matibabu wakati wanapougua lakini pia itawawezesha kuepukana na kutumia fedha nyingi pindi wanapokuwa wakiugua zinazotokana na kupanda kwa gharama.
“Ndugu zangu maradhi yanakuja bila taarifa hivyo iwapo tutawekeza kujiunga na mpango wa Mfuko huu unaweza kufaidika na matibabu lakini pia utaepukana na gharama kubwa za matibabu utakazopaswa kulipia wakati unapokumbana na magonjwa mbalimbali “Alisema.
Hata hivyo Sophia alisema pia wanatumia nafasi hiyo kuendelea kuhamasisha wazazi na walezi kuwapa watoto wao uhakika wa matibabu wanapokuwa wakiugua kwa kuingiza kwenye mpango wa Toto Afya kadi ambao utamuwezesha kupata huduma.
“Ndugu zangu lazima tuona namna bora ya kuwapa zawadi nzuri ya matibabu kwenye msimu huu kwa kuwaingiza kwenye mpango wa Toto Afya Kadi kwani hii itawawezesha kupata uhakika wa matibabu pindi wanapoumwa”Alisema.
Maonyesho hayo ambayo yalifunguliwa jana na Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage yamebeba kauli mbiu isemayo Biashara ndio ufunguo wa Tanzania ya Viwanda (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6XoMEa433983EPpiHHORr6G2sJ830QjEMK5RTO2cpxBMEhV6eQ7Uzi5j7utTwt1U0EapJmgRIS_OMJwAxLPiwkXYDF2_15a0ZX6t7oEp8knKZsFkW-g-RPWfaE3I-_5tdjRk5Sw2mSkg/s640/IMG-20180528-WA0011.jpg)
Sehemu ya wananchi Jijini Tanga wakiingia kwenye banda la NHIF kupata huduma za upimaji wa afya zao na namna ya kujiunga na mfuko huo
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-4nE1OZkPIfNn-TltUXFeUtfSMv3tqMvR0p5yQSsCJmREa6FVZc-GG-GYEFqhkPBb37pkGncs_-r3ZvjHFoDWtPviz9CJpmcuG_juI11A1rx_0pFdNUHKRpvbSzW8LL9bk77knFONcBs/s640/IMG-20180528-WA0008.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgeCp-T72Wk03FC1JzxEks9xnVuYxbSoyafy7aFSQDO0Kbz7CLJLUgRzMOrFydDU36RbVjWmgzubhRkW9bVF1OlGoAn7rG0AYWvqHI45qNax9QrdOU72tAUMG13jmcFAWojd8fjQYdMjKI/s640/IMG-20180528-WA0010.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiJzmX358MQReVUFNTZVlJujND-uWvzp9xWxiJKukbpb5qz47L-Pr5qk-FQVHC5qOLQkut-9A5IkrYReitxVBIJ84QQfhix72eZS4Yyn6ZGs1mqu2jurfViUfBnEKtNl9e7QNOZX4WYMNY/s640/IMG-20180528-WA0009.jpg)
No comments:
Post a Comment