Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imezindua mpango wa ufadhili wa masomo
ujulikanao kama Sanaa tuition fee waiver scholarship kwa wanafunzi 20 kwa mwaka
wa masomo 2018/2019.ambapo kwa upande wa Tanzania ufadhili huo utahusu
wasichana 10 ,wanafunzi wengine kumi watatoka nchi wa washiriki wa jumuia ya
Afrika Mashariki.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo wilayani Bagamoyo, Mtendaji mkuu wa
TaSUBa Dkt.Herbert Makoye amesema “Taasisi imekuja na mkakati wa kutoa ufadhili
wa ada ya masomo ili kuweza kuziba mapengo makubwa mawili ambayo yamedhihirika
katika utoaji wa mafunzo. Kwanza kuna uwiano hasi kati idadi ya wanachuo wa
kike na wale wa kiume.
Wanachuo wa kike wanaodahiliwa kila mwaka na Taasisi ni
wachache sana (chini ya 30%) ikilinganishwa na wa kiume. Pili, pamoja na kupata
hadhi ya kuwa kituo cha ubora uliotukuka kwenye ufundishaji katika nyanja za
utamaduni na sanaa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Taasisi haijaweza
kudahili wanachuo kutoa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.”alisema
Makoye
Aliongeza
kuwa malengo makuu ya utoaji wa Ufadhili
wa ada ya masomo ni Kuwezesha vijana wa kike wa Kitanzania wenye vipaji vya
sanaa kupata nafasi ya kunoa vipaji vyao kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa
kwenye Taaisisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Lakini pia ni fursa
kwa Taasisi kujitangaza nje ya mipaka ya Tanzania na kuingia katika soko na kuuza bidhaa zake kwa raia wa nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki
Naye
mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TaSUBa ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi kwenye
uzinduzi huo Ndg.George Daniel Yambesi aliishukuru TaSUBa kwa ufadhili huo Kwa kuwa umeonyesha njia, kwa sababu ni
kweli kabisa kuwa kuna vijana wengi wenye vipaji hasa wa kike ambao hawana
uwezo wa kulipia gharama za masomo.
Aidha ndugu Yambesi aliitaka TaSUBa ihakikishe ufadhili huu kweli unakwenda kwa walengwa; yaani
vijana wenye vipaji vya sanaa na wana uhitaji wa ufadhili. Kwa kufanya hivi
matunda ya ufadhili huu yataweza kweli kuonekana baada ya vijana hawa kuhitimu
masomo yao.
Wakati huo huo ,baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) pamoja na Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza zimejitolea kufadhili
malazi na Chakula kwa kipindi chote cha masomo kwa wanafunzi kumi wa kike kutoka
Tanzania watakao faidika na ufadhili huo.
Uzinduzi huo ulisindikazwa na onyesho
la ngoma za asili kutoka TaSUBa na Muziki kutoka kwa Jhikoman na Afrikabisa
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya
TaSUBa Ndugu George Daniel Yambesi
,akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Bi.Edda Sanga akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
. Mwenyekiti wa chama cha wabunifu mitindo Ndugu.Merinyo Desumbuka akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Mwakilishi kutoka Basata Ndugu Onesmo Kayanda akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Onyesho la ngoma za asili kutoka TaSUBa
Onyesho la Muziki kutoka kwa Jhikoman na Afrikabisa
Mwenyekiti
wa bodi ya ushauri ya TaSUBa Ndugu
George Daniel Yambesi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa tasuba
pamoja na waalikwa
No comments:
Post a Comment