Thursday, October 05, 2017

WANANCHI MALINYI WAMLALAMIKIA DC KUCHELEWESHA MRADI WA MAJI

Na Mwandishi wetu

Wananchi wa kijiji cha kwa Misegese mkoa wa Morogoro Wilaya ya Malinyi wamemlalamikia mkuu wa Wilaya hiyo Majura Kasika kwa kukwamisha mradi wa uchimbaji kisima katika kijiji cha kwa madai ya kuomba apewe fidia katika ardhi aliyopewa na kijiji.

Wakizungumza na Mwandishi wa Globu ya Jamii baadhi ya wanakijiji wa eneo hilo wamedai kuwa licha ya Rais kutoa pesa za kuchimba visima 25 katika Wilaya hiyo yenye thamani ya Zaidi ya Milioni 538 lakini Dc huyo amekuwa mtu wa tofauti kutokana kupinga mradi wa maendeleo katika eneo lao.

“sisi tunashanga Mkuu huyu wa Wilaya tulimkaribisha wenyewe hapa na kumpa ardhi kwa heshima lakini yeye leo watu wamepima wamekuta kwenye ardhi anayomiliki yeye ina maji sasa anatudai fidia ama kisima kisichimbwe katika Kijiji chetu” Amesema Mkazi huyo.

Nae mmiliki wa kampuni inayochimba Visima Wilayani Malinyi,Bhaskar amekiri kuwa aliitwa Wilayani hapo kwa ajaili ya mgogoro huo ambao ulipelekea kusimama kwa kazi kwa Zaidi ya saa 24. Bhaskar anasema kuwa Dc alimwambia alipe fidia au amchimbie kisima cha bure pembeni ya eneo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Majura Kasika amesema kuwa yeye ajazuia bali aliwaita ofisini kwake kuwauliza kwanini wanachimba bila ya kumpa taharifa ndipo walipozungumza na kufikia muafaka wakakubaliana watamchimbia kisima pembeni kisha atalipa Milioni 4 kama gharama za mabomba madomadogo.

Amesema kuwa Shamba hilo yeye alinunua kwa mwananchi na ajapewa na Kijiji hivyo alitakiwa apewe taharifa kabla ya zoezi la uchimbaji alijaanza

No comments:

Post a Comment