Wednesday, October 18, 2017

NAIBU WAZIRI KAKUNDA AFANYA ZIARA KILWA


PICHANI: Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo kulia akitoamaelezo ya mradi mkubwa wa uoteshaji wa miche ya korosho kwa Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai

Pamela Mollel, Kilwa

Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda amewataka viongozi wa serikali wilayani Kilwa Mkoani Lindi kuhakikisha wanasimamia vyema upandaji wa miche mipya yazao la korosho hali ambayo itaongeza uzalishaji wa zao hilo kwa wananchi na kuinua uchumi wa Taifa

Hayo aliyasema jana wilayani Kilwa wakati wa ziara yake baada ya kuelezwa kuwa mkakati wa wilaya uliopo ni kuhakikisha wanazalisha na kupanda miche milioni moja kila mwaka hali ambayo itaongeza mashina ya zao hilo kutoka laki sita yaliyopo na zaidi kutokana na mpango huo kuwa wakudumu

Kufuatia hali hiyo Kakunda alisema ili miche hiyo iote vizuri na kustawi lazima uwepo usimamizi mkubwa kwa viongozi wote wa serikali wilayani humo kuliko kuacha usimamizi kwa wakulima peke yao ambao wanaweza kusababisha kukauka na kushindwa kufikia malengo

Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo alisema tayari hatua za awali za kuotesha miche milioni moja kila mwaka zinaendelea ambazo miche hizo itagawiwa bure kwa wakulima hali ambayo itainua uchumi wao

Bugingo alisema mpango huo ni wakudumu ambapo kila mwaka wilaya itazalisha miche hiyo milioni moja na kuigawa kwa wakulima bure hali ambayo itakuwa zaidi ya mara mbili ya uzalishaji wa miche iliyopo ambayo kwa sasa ni laki sita tu iliyowaingizia shilingi Bilioni 13 na halmashauri kujipatia zaidi ya shilingi milioni220

Aliongeza kuwa mbali na kujipatia fedha kwa wakulima pia halmashauri itajiongezea mapato ya ushuru baada ya serikali kufuta baadhai ya vyanzo ikiwemo ya mabango iliyorudishwa serikali kuu hivyo zao hilo la korosho linaweza kuingizia halmashauri zaidi ya shilingi bilioni 40 kutokana na mpango huo kuwa zaidi ya mara mbili zaidi

Mbali na hali hiyo Waziri Kakunda ameupongeza mpango huo wa upandaji wa miche hiyo milioni moja kila mwaka kutokana na kuvuka malengo ya serikali ya kupanda miche elfu 50 kwa kila wilaya inayolima zao la korosho ingawa Afisa kilimo na ushirika wa halmashauri hiyo ya Kilwa John

Mkinga amesema changamoto iliyopo ni ucheleweshwaji wa mbegu hali inayosababisha zoezi la uoteshaji miche hiyo kwenda taratibu ingawa Kakunda amesema atawasiliana na wizara ya kilimo kumaliza tatizo hilo







Afisa kilimo na ushirika wilaya ya Kilwa John Mkinga kushoto akitoa taarifa ya mradi wa uoteshaji wa miche ya korosho mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo







Picha ikionyesha viriba vya kuoteshea miche ya korosho



Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda akiingia katika eneo la uoteshaji wa miche ya korosho,kushoto ni Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai









No comments:

Post a Comment