PICHANI: Meneja Tukio wa Tamasha la Dimba Concert , Mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Tamasha litakalo wakutanisha Wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini na bendi ya Msondo Ngoma katika ukumbi wa Traventine September 2 mwaka huu kwa kiingili cha shilingi 10,000 na 20,000 kwa VIP.
Na Agness Francis,Globu ya Jamii
Wanamuziki wakongwe wa Muziki wa
Dansi nchini wametambiana kuoneshana uwezo wa kuimba siku ya Tamasha la
Dimba Concert litakalofanyika katika ukumbi wa Traventine Magomeni
Septemba 2 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam meneja tukio tamasha la dimba concert,Mwani
Nyangasa amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa
Taifa muziki bendi kupambana na wanamuziki nguli wa Bendi ya Msondo
ngoma.
“ dhumuni la tamasha hili ni kuendeleza muziki wa dansi
hapa nchini kwa kutumia wasanii hawa wakongwe ili waweze kuonesha
vijana,wapenzi na wadau kuwa muziki huu bado upo hai.” Amesema
Nyangasa.
Nae msanii nguli nchini Hussen Jumbe ametanabaisha
kuwa wadau na mashabiki wa muziki huo wafike kwa wingi siku hiyo pale
Traveltine septemba 2 mwaka huu ili kupata radha halisi ya muziki wa
dansi.
Kwa upande wake raisi wa vijana sauti ya simba Nyoshi El
Saadat, amewaomba mashabiki wa muziki huo kufika kwenye tamasha hilo
na kuwaahidi kutowaangusha na kuwapa burudani ya kukata na shoka.
Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Tanasha la Dimba Concert , Jimmy Chika akifafnua namna bendi hizo zitkavyotoa burudani kwa mashabiki na wadau wa Muziki wa dansi watakaofika katika ukumbi wa traventine siku ya Jumamosi
Msanii wa Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini, Husein Jumbe akiwatoa hofu Mashabiki wake kuwa muziki wao bado upo juu
Mwanamuziki wa Mkongwe wa Double M Sound , Mwinyjuma Muumini akijgamba kwa tambo kuwa siku hiyo patachimbika kwa hiyo mashabiki wote wasikosekuhudhuria Tamasha hilo
Mpiga gitaa la solo wa siku nyingi , Adolf Mbinga akionyesha namna atakavyocharaza nyuzi siku ya Tamasha la Dimba Concert siku ya jumamosi
Mwanamuziki Juma Kakere akieleza namna watakavyoweza kukonga nyoyo za Mashabiki kupitia nyimbo zake kadhaa ambazo ziliweza kutamba
Rais wa Vijana wa Muziki wa Dansi nchini , Nyoshi Elsadat akieleza namna atakavyoweza kutoa burudani kwa wadau wa muziki wa Dansi na Mashabiki watakaofika siku hiyo
Wanamuziki wakongwe wakiwa katika mazoezi yao wakionyesha namna watakavyoimba siku ya Dimba Concert siku ya Jumamosi
Rais wa Vijana wa Muziki wa Dansi nchini , Nyoshi Elsadat akiimba mbele ya waandishi wa habari namna atakavyofanya siku ya Dimba Concert itakayofanyika Sept 2 mwka huu katika ukumbi wa Traventine Magomeni
No comments:
Post a Comment