Leo June 20, 2017 watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
wameanza kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano
mkubwa uliohudhuriwa na watumishi wote wa makao makuu katika ukumbi wa
Manispaa hiyo mkutano ambao umeongozwa na Afisa Utumishi Mkuu wa
Manispaa hiyo Ndg Ally Juma Ally kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo.
Akiongea
katika kikao hicho mara baada ya kufungua kikao Afisa Utumishi mkuu
aliwajulisha kuanza rasmi kwa wiki ya utumishi na kutoa utaratibu wa
jinsi Halmashauri itakavyotimiza maadhimisho hayo ambapo alisema kuwa
kwa wiki hii ya maadhimisho muda wa kutoka kazini utaongezeka kwa saa
moja badala ya kutoka saa tisa na nusu mchana itakuwa ni saa kumi na
nusu, hali kadhalika alisisitiza mambo ya kuzingatia katika wiki hii na
hata baada ya maadhimisho no pamoja na Kufanya kazi kwa kuzingatia
sheria,kanuni taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma,
Kufanya kazi zetu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, na Kufanya
kazi kwa uadilifu mkubwa bila ya viashiria vya kupokea rushwa au hongo
katika kutoa huduma katika ofisi za serikali au umma.
Mengine
ni Kuongeza Ari na kujituma katika kutekeleza majukumu yetu, Kufanya
kazi kwa maarifa na kuwasikiliza wanaanchi wanapofika kupata huduma
katika ofisi za umma/serikali na Kuweka vizuri kumbukumbu za wananchi
watakaohudumiwa kwa kipindi hiki ili kuzitolea taarifa kwenye mamlaka
husika.
Pia wamesisitizwa kutoa
Huduma bora, Utii kwa serikali, Kuongeza bidii ya kazi, Kutoa huduma
bila upendeleo, Kufanya kazi kwa Uadilifu, Uwajibikaji kwa Umma,
Kuheshimu sheria na taratibu za kazi, na Matumizi sahihi ya Taarifa.
Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Mariam Maliwa akifatilia kwa karibu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Afisa Utumishi Manispaa ya Ubungo Ndg Alute Joseph akitoa ufafanuzi wa kanuni za maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
No comments:
Post a Comment