PICHANI: Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake. (Picha zote na Nassir Bakari)
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo imebainisha namna ya kuboresha maisha ya wakazi wake kwa kuweka
mpango mzuri wa muda wa kati wa mwaka 2017/2018 – 2019/2020 ambao
unalenga kukuza uchumi, na kupunguza umaskini ili kufikia maendeleo
endelevu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa wananchi wake.
Mpango
huo umeandaliwa kwa kuzingatia sera na miongozo ya Kitaifa, kwa mujibu
wa sheria ya bajeti Na. 11 ya mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo
2025 ambapo Mpango mkakati ni kutekelezwa kwa matokeo makubwa sasa
(BRN), Sera ya Taifa ya UKIMWI, Sera za kisekta, Mipango Shirikishi
Jamii ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) ya Kata na Mitaa.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo
Mhe Boniface Jacob alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake kuelezea juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya kawaida na ya
maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018, Makadirio yalijadiliwa na
Waheshimiwa Madiwani katika Kamati za Kudumu,na kuidhinishwa na baraza
maalumu la madiwani jumamosi ya tarehe 04/03/2017 kwa katika Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo.
Mstahiki Meya alisema kuwa ili
kutekeleza dhana nzima ya ung’atuaji wa madaraka, mpango huu
umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi ambao huanzia ngazi ya Mtaa
ambapo Hali hiyo imezingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi
katika maeneo yao.
Alisema kuwa Mpango huo umejielekeza katika
kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo ya haraka (quick wins)
ambayo yatasaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka katika kipindi kifupi na
kutoa huduma bora kwa wananchi wa Ubungo.
Aidha alieleza maeneo
yaliyopewa kipaumbele katika mpango huo kuwa ni pamoja na Kuboresha na
kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Manispaa, Ujenzi wa ofisi za makao
makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Kuboresha miundombinu ya
Afya, Shule za Msingi na Sekondari, Kuboresha miundombinu ya maji,
mifereji, taa za barabarani barabara na Kilimo mjini, Kuboresha hifadhi
ya mazingira na ukusanyaji wa taka, Kuimarisha ushirikishwaji wa jamii
katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Kuboresha
mazingira ya wafanyabiashara ndogo ndogo.
Katika harakati za
kuyafikia mafanikio yaliyotajwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa
ya Ubungo ameeleza kuwa Manispaa hiyo Uimarisha mahusiano mazuri kati
ya Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali na wadau wengine, Kuendelea
kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma zilizo bora
na haraka, Kuimarisha Utawala bora, Uwajibikaji na Uwazi sambamba na
Kujenga uwezo wa viongozi wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa serikali za
mitaa katika kusimamia shughuli za wananchi.
Sambamba na hayo pia amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa mwaka 2016/2017 ilikadiria kutumia Sh. 116,045,935,228.99 ikiwa ni pamoja na fedha za mfuko wa barabara.
Kuanzia
Julai hadi Disemba, 2016, Halmashauri ilikuwa imekusanya Sh.
1,024,839,737.74 fedha za vyanzo vya ndani sawa na asilimia 8 ya maoteo
ya Tsh 13,300,416,090.50 ya vyanzo vya ndani yaliyotarajiwa kukusanywa
kwa nusu mwaka wa bajeti yaani Julai 2016 hadi Disemba 2016.
Katika
kipindi hiki Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeweza kutumia kiasi
cha Sh. 150,764,997.88. ya makusanyo yake ya ndani yaliyoanza kukusanywa
mwezi Novemba 2016, na hakuna fedha yoyote ya ruzuku iliyopokelewa
hadi sasa kama inavyooneshwa katika Jedwali hapa chini.
Jacob
ametaja changamoto mbalimbali zinazopelekea ucheleweshaji katika kutoa
huduma na kuleta maendeleo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na Mwamko mdogo
wa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo, Fedha za miradi za Serikali
kuu na wafadhili kutoletwa kwa wakati na hivyo kuathiri utekelezaji wa
miradi kama ilivyopangwa. Miradi yote iliyopangwa kutekelezwa kwa fedha
za ruzuku haijaanza, Makusanyo hafifu ya mapato ya ndani kutokana na
mgawanyo wa Halmashauri na upya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Hivyo miradi iliyopangwa kutekelezwa kwa mapato ya ndani mingi
haijaanza kutekelezwa, Ukosefu wa maeneo ya kujenga majengo mapya kama
vile Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na Madai makubwa ya fedha za
fidia katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo Sababu zilizopelekea
kukusanya mapato ya ndani chini ya malengo ni pamoja na Serikali
kuhamishia kodi ya Majengo kukusanywa na Mamlaka ya mapato TRA ambapo
kwa wigo wa makusanyo uliopo wa kodi ya majengo ni shilingi bilioni 6,
kwa bajeti ya mwaka 2016/2017 ya makusanyo ya ndani yenye makadirio ya
Tsh. 26.6 bilioni, Kushuka kwa mauzo ya wafanyabiashara hali
inayopelekea biashara kufungwa na malipo ya ushuru wa huduma kupungua,
na SUMATRA kubadilisha route za mabasi ya kariakoo (160) na mikoani
(350) kimepunguza makusanyo katika kituo chetu cha Simu 2000 (Sinza bus
terminal) ambapo takribani magari kati ya 510 yaliyokuwa yanaingia
kituoni yamepungua na kusababisha upungufu wa Sh. 12,900,000/= kwa kila
mwezi.
Sababu zingine ni Upungufu wa vitendea kazi baada ya
Mgawanyo wa Halmashauri na hasa ukosefu wa magari yanayotumika
kukusanyia mapato, Kipindi cha mpito tangu kuanzishwa kwa Halmashauri
hadi kuanza kukusanya mapato ya ndani kwa Halmashauri yetu mpya
ilipoanzishwa rasmi tarehe 1/07/ 2016, imeanza kukusanya mapato yake ya
ndani yenyewe kuanzia mwezi Novemba 2016, Walipakodi kuendelea kulipia
katika Halmashauri mama (Kinondoni) kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba
2016 kwa mazoea kiasi cha takriban Sh. milioni 500 kimekusanywa kimakosa
na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni mawasiliano yanafanyika ili
kurejesha makusanyo hayo.
Ili kukabiliana na changamoto hizo
Mikakati ya Halmashauri imetajwa kuwa ni pamoja na Kuendelea kutoa elimu
na kuhamasisha wananchi ili kutambua kuwa miradi ya maendeleo
wanayochangia ni kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na vizazi vijavyo,
Kendelea kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya
kwa mujibu wa sheria na kuimairisha ukusanyaji wa mapato katika vyanzo
vilivyopo.
Mikakati mingine ni Kukusanya mapato yote kwa kutumia
mfumo wa kielektroniki, na Kununua maeneo ya pembezoni mwa mji na
kuhakikisha tunalipa fidia kabla ya kuyatwaa maeneo ya watu.
Vipaumbele
vitakuwa katika maeneo yafuatayo:-Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo
Mhe Boniface Jacob amebainisha kuwa Bajeti hiyo imelenga katika
kuboresha maisha ya wananchi na kukuza kipato cha mkazi ili kukuza
uchumi wa ndani ambapo ametaja vipaumbele 13 ambavyo vitapaswa kufanyiwa
kazi katika bajeti hiyo kuwa ni pamoja na Kuongeza ukusanyaji wa mapato
ya ndani kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, na Kuboresha utoaji wa
huduma za afya kwa kununua madawa na vifaa tiba na kuboresha miundo
mbinu ya afya kwa kupanua hospitali ya Sinza kwa kujenga ghorofa ya pili
jengo la OPD, Ujenzi wa wodi ya wazazi kituo cha afya mbezi, ujenzi wa
jengo la kuhifadhia chanjo Mabibo, kujenga zahanati ya King’azi Kwembe
Jumla ya Tsh. 5,732,424,610.00 zimetengwa.
Kuboresha
miundombinu ya barabara kwa kujenga Madaraja/ Makalvati, barabara kwa
kiwango cha lami, kufanya matengenezo ya kawaida ya barabara, muda
maalum, maeneo korofi, njia za waenda kwa miguu, Ujenzi wa Mifereji
katika barabara za Manispaa ambapo Jumla ya Tsh 6.2 bilion zimetengwa,
Kuboresha miundo mbinu ya shule za Msingi na Sekondari kwa kununua
madawati, kujenga madarasa, vyoo, nyumba za walimu, maabara na ukarabati
wa miundombinu. Jumla ya Tsh.5.5 billion zimetengwa na Kutoa mikopo kwa
wajasiliamali wa dogo kwa vikundi vya wanawake na vijana ili kuongeza
ajira na kukuza kipato cha Mkazi. Jumla ya Tsh.1.9 billion zimetengwa.
Kuboresha
mazingira ya kufanyia kazi na kutoa huduma kwa kujenga Ofisi za
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Tsh.1.7 billion zimetengwa, Kununua
magari na mitambo magari 6 ya ofisi, gari moja la maji machafu na gari 1
la maji safi, jenereta. Jumla ya Tsh 1.35 billion zimetengwa, Kulipa
fidia kupisha ujenzi wa miradi mabali mbali ya maendeleo na kufanya
uthamini wa mali za Manispaa. Jumla ya Tsh.1.2 billion zimetengwa,
Kuboresha usafi wa mazingira na na ukusanyaji taka na kununua magari
makubwa ya taka Jumla ya Tsh.1 billion zimetengwa, Kuboresha upatikana
maji safi na salama kwa wakazi wa Ubungo kwa kujenga na kukarabati
miundo mbinu ya maji. Jumla ya Tsh.550 million zimetengwa kwa ajili ya
ujenzi wa miradi ya maji na Mipango miji, kupima na kumilikisha maeneo
ya umma na kutekeleza mfumo wa anuani za makazi (Postcode). Jumla ya
Tsh.550 million zimetengwa.
Aidha Halmashauri ya Maninspaa ya
ubungo imetenga Tsh 42 milioni kwa mwaka huu kwa ajili ya kijiji cha
michezo kilichopo kibwegele ambapo kijiji hicho kitakuwa na kiwanja cha
mpira wa miguu na viwanja vya michezo ya watoto, kwa Mwaka wa fedha
2017/2018 ambapo Tsh 50 milioni zimetengwa, na Kuboresha na kukarabati
masoko Manispaa tumetenga Tsh 1.2 Bilioni, kwa ajili ya kuboresha masoko
ambayo ni Mabibo, Shekilango, Sinza one, na Mbezi pia fedha hizo
zitatumika kulipa fidia na kupima maeneo kwa ajili ya wamachinga na
maeneo ya uwekezaji.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea Makadirio ya Mapato na Matumizi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akielezea jinsi Bajeti ya Manispaa hiyo ilivyopitishwa kwa kuungwa mkono kwa 100% kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kilichofanyika 4/03/2017.
No comments:
Post a Comment