PICHANI: Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela(katikati) akionyesha kwa waandishi wa habari bia mpya ya chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki., kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha na Meneja kiwanda Dominic Mkemangwa.
Mwanza, Machi 8, 2017- Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella leo
ameipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kuzalisha bidhaa zenya
ubora wa hali juu jambo ambo limiweizesha kampuni hiyo kushinda tuzo
mbalimbali za ubora ndani na nje ya nchi.
Mongella alitoa kauli
hiyo wakati alipokitembelea kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza ambako
pia aliipongeza kampuni kwa mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi
ya nchi kupitia uzalishaji wa ajira, ulipaji kodi na hali kadhalika
programu za kusaidia jamii.
“SBL ni mdau katika ajenda ya
maendeleo ya nchi yetu. Kama serikali tutajaribu kuanzisha mazingira
ambayo yanawezesha biashara kama hii ili istawi vizuri na kuvutia
uwekezaji pia,” alisema Mongella.
SBL inazalisha chapa za bia
ambazo ni Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, TuskerLite,
Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick na hali kadhalika kusambaza
pombe kali zinazofahamika duniani ambazo zinazalishwa na kampuni yake
uwekezaji Diageo.
Mwezi uliopita Kiwanda cha SBL cha
Mwanza kilianza uzalishaji wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika
soko la Afrika mashariki.
“Hatua ya kuzalisha Allsopps katika
kiwanda chetu cha Mwanza ni sehemu ya mbinu ya uendeshaji kikanda ya
EABL. Hili limekuwa na matokeo ya kunufaisha kwa masoko yote na kwa
biashara yetu,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John
Wanyancha.
Kwa mujibu wa Wanyancha, SBL inaendesha miradi kadhaa
ya kuisaidia jamii nchi nzima katika maeneo ya upatikanaji wa maji,
utoaji wa elimu- ambapo wanafunzi walio na weledi mkubwa kutoka
mazingira yenye uhitaji hupatiwa udhamini wa masomo kwa ajili ya
kusomea kozi za shahada ya kwanza katika vyuo vikuu vya ndani na hali
kadhalika kampeni ya Ukiwa Umekunywa Usiendesha gari ambayo
inahamasisha unywaji wa kistaarabu.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akifafanua jambo jijini Mwanza jana wakati wa uzinduzi wa bia mpya ya Allsopps, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL na waandishi wa habari mara baada wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akiongozana naviongozi wa SBL na waandishi wa habari maeneo ya kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza mara baada ya uzinduzi wa wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.
No comments:
Post a Comment