Kampuni lisilo la kiserikali "Namaingo Business Agency" ukanda wa Mbeya leo katika Kata ya Manga ,mtaa wa Maendeleo limefanya mkutano wa mafunzo kwa wananchi wa Kata hiyo na maeneo ya jirani wakiwa na malengo makuu ya Kuifundisha jamii mbinu mpya na bora katika kuyaendea mafanikio binafsi na kupunguza utegemezi.
Akiongea kwa umaridadi mkubwa Bw.Gaudence Rwabyoma juu Pichani ambaye ni Mkufunzi wa masuala ya Uchumi ndani ya Namaingo ameutanabaisha Umma kwa kutumia mifano mtambuka kuwaeleza makumi ya wananchi waliokuwepo mkutanoni hapo mbinu mpya ya kufikia maendeleo hasa kwa kutumia mfano wa jinsi gani Serikali, mkulima, mnunuzi, taasisi za kifedha, mtaalamu na mwanasheria wanavyoweza kutegemeana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuzalisha zaidi.
Mkufunzi huyo ameutanabaisha Umma kuwa wao kama Namaingo wanafanya kazi kwa kushirikiana zaidi na serikali hivyo ni nafasi ya wananchi kukipatia maeneo mengi ya ardhi ya kuanzisha Vijiji mradi kwa kupata ekari nyingi za uwekezaji, pia Namaingo kuhakikisha wananchi wanapata mitaji kwa riba nafuu na masoko pia.
Bw.Gaudence amesema kupitia kujiunga na Kampuni hiyo kutamwezesha mwananchi wa kipato cha chini kujiunga na baadhi ya taasisi kwa urahisi zaidi ikiwepo Shughuli za usajili wa kampuni zao Brella, kupata utambulisho wa Biashara TIN na kupata Leseni kwa haraka na wepesi.
Pia mwana Namaingo atakatiwa Bima ya Biashara ili gata ikitokea kakopeshwa Milioni 5 na mwananchi akaamua kufuga kuku ,ghafla ugonjwa ukatokea kuzishambulia kuku mteja huyo atalipwa ili kuendelea na ufugaji wake pasipo kugharamia tena.
Akiongea na mkutano huo Diwani wa kata hiyo Mh.Newton Mwatujobe ameitaka Kampuni hiyo kuhakikisha ina wasaidia zaidi wananchi waweze kufikia mafanikio yao bila kupata usumbufu kwa baadhi ya mambo yenye changamoto kubwa kama Suala ls usajili Brella, kupata TIN na Leseni.
Naye Mratibu wa Namaingo Business Agency Mkoa wa Mbeya Bw.Jottam Willson huku akimkaribisha Kiongozi mwenza wa Namaingo-Mbeya Bi.Zenobia Ishika ili kuwashukru wananchi amewaomba wananchi wote kuitembelea Kampuni iyo kwani ni yao wananchi na pindi wawapo na maswali ya hapa na pale basi wasisite kufika Ofisi zao Zilizopo Mtaa wa Block T, Kata ya Iyela karibu na Shule ya sekondari ya Southern Highland na Chuo Kikuu Teofilo Kisanji (TEKU) kwa upande wa Mashariki mwa Ofisi yao.
Bi.Zenobia Ishika alimalizia kwa kuwashukuru wananchi kwa Uvumilivu na Utulivu waliouonesha muda wote wa Mkutano na kuwatakia utekelezaji mwema wananchi pamoja na kuwauzia baadhi ya Machapisho yahusuyo Sheria ya Ardhi na Namna bora ya Uandishi ya Urithi na mirathi.
Mama huyu mkazi wa Jijini Mbeya akiwa ametulia na kumsikiliza kwa makini Mkufunzi wa Namaingo Bw.Gaudence Rwabyoma
Mkufunzi wa Uchumi wa Namaingo Bw.Gaudence Rwabyoma akielekeza jambo kwenye mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Manga Jijini Mbeya
Bw.Gaudence Rwabyoma akisisitiza jambo wakati akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa Wakazi wa Kata ya Manga Jijini Mbeya
Elimu ni Bahari, Elimu haina mwisho!! Wazee wakiendelea kuifaidi Elimu ya bure iliyokuwa ikitolewa na Kampuni ya Namaingo Business Agency
Bw.Thobias Omega (wa kwanza kulia) mwanaHabari wa Blog hii akifuatilia mafunzo na kuandika mambo muhimu
Akina Mama nao hawakua mbali kwenye mafunzo, Elimu hii ni elimu yenye manufaa hivyo utulivu ulitawala
ELIMU KWA VITENDO: Baadhi ya wakazi wa Kata ya Manga wakionyesha jinsi Namaingo inavyofanya kazi kwa kuwaunganisha Serikali,Wakukima/wafanyabiashara, wanunuzi, taasisi za kifedha,wataalamu na wanasheria
Elimu ikiwa imewakolea kina mama wakati wakufunzi wa Namaingo wakiendelea kufundisha na kujibu maswali
Bi.Zenobia Ishika mmoja wa viongozi waandamizi wa Namaingo Jijini Mbeya akimsikiliza Mwezeshaji wa Semina waliyofanya kwa wananchi Jijini Mbeya
Diwani wa Kata ya Manga Mh.Newton Mwatujobe akissisitiza jambo kwa wananchi kuonyesha kuridhishwa na huduma zitolewazo na Kampuni ya Namaingo
Bw.Jottam Willson akiwashukuru wananchi wa Kata ya Manga kwa kuwakaribisha vizuri na kudumisha utulivu muda wote wa Mkutano huo
Wakufunzi kutoka Namaingo Jijini Mbeya katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kata ya Manga na Wakazi wa Mtaa wa Maendeleo
No comments:
Post a Comment