Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo(picha na woinde Shizza wa libeneke la kaskazini Arusha)
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiwa anahubiri katika hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha hii leo
Habari picha na woinde shizza,Arusha
Watumishi wa
madhehebu mbalimbali hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya
kuwasaidia yatima ili nao waweze kujisikia kama wao ni sehemu ya jamii
Hayo
yamebainishwa leo na Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie wakati akifanya
dua maalumu ya kupitisha bajeti ya watu walioshiriki katika sikukuu ya
kukusanya iliyofanyika katika hema la kukutania ngurumo ya upako
kisongo jijini Arusha.
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtumishi
kukusanya na kutoa kile alichonauwezo nacho ili kuweza kuwasaidia
watoto yatima ,wananchi wasiojiweza ili kuweza kuwafanya nao wajisikie
ni sehemu ya jamii
Alisema kuwa mbali na watoto yatima pia
aliwasihi makanisa ambayo yanajiweza kuweza kusaidia yale ambayo ni
machanga ili kuweza kuwapa nguvu ya kuweza kuendelea kueneza injili na
kumtangaza mungu kupitia makanisa yao .
Nabii mkuu Dr Geordavie
alisema kuwa kuwa lengo la sikukuu hii ya kukusanya nikuwasaidia
watoto yatima kwa kuwapa chakula kama mchele, sukari pamoja na mafuta
yakupikia ili nao wajisikie wanafuraha haswa katika kipindi hichi cha
sikukuu.
Alisema kuwa licha ya misaada hiyo kwenda kwa watoto
yatima, pia atatoa fedha kwa watumishi wa mungu wenye makanisa madogo
hapa nchini lengo likiwa ni kuinua huduma zao na kuwasaidia katika
kuendeleza huduma zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kanisa, ununuzi wa
vyombo vya muziki na shughuli nyingine za kanisa.
Sikukuu hii ya
kukusanya huadhimishwa na huduma ya Ngurumo ya Upako Duniani tarehe 26
ya kila mwaka, watu hutoa sadaka ya vitu mbalimbali ikiwemo fedha kwa
mujibu wa maelekezo ya Nabii Mkuu na kisha hugawanywa kwa vituo vya
watoto yatima huku fedha zikigawanywa kwa watumishi waliotuma maombi
ya kupata msaada wa kuendeleza huduma zao.
Mwaka jana msaada wa
zaidi ya shilingi milioni 15 ulitolewa na waumini wa kanisa la Ngurumo
ya upako na kugawanywa katika vituo mbalimbali vya watoto yatima huku
fedha zikigawiwa kwa baadhi ya makanisa madogo kwa ajili ya kuwasaidia
mambo mbalimbali .
Nabii mkuu akiwa anaendelea na huduma ya sikuu kuu ya kukusanya hii leo
Nabii akiwa anamwaga upako kwa waumi waliouthuria katika siku kuuu hii ya kukusanya hii leo (picha na Woinde Shizza,Arusha )
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo
No comments:
Post a Comment