Thursday, August 11, 2016

WADHAMINI WARUDISHA HADHI YA SHINDANO LA MISS TANGA 2016


Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kushuhudia shindano hilo mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi


Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono watazamaji waliojitokeza akiwa na mshindi wa pili na tatu katika Shindano hilo ambalo liliandaliwa na Radio Tanga Kunani (TK) na Hotel ya Tanga Beach Resort.

Warembo walioingia tano bora wakiwa jukwaani


Kamati ya Miss Tanzania nao walikuwepo wakifuatilia shindano hilo ambalo lilifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.


Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akizungu mza wakati wa shindano hilo


Msanii Nevy Kenzo akitumbuiza wakati wa shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)lililofanyika hivi karibuni kwenye hotel ya Tanga Beach Resort



WAKATI shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)likifanyika mwishoni mwa wiki na hatimaye mrembo Eligiva Mwasha kuibuka na ushindi kwenye kinyang’anyiro hicho dhidi ya washiriki wengine 10.

Shindano hilo ambalo lilisimama kwa muda baada ya serikali kulisimamisha lile la Taifa msimu huu lilionekana kuwa na msisimuko wa hali ya juu kuanzia wapenzi,wadau na washiriki iliyochangiwa na waratibu wa shindano hilo Radio ya Tanga Kunani FM (TK) wakishirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort. 

Ushindani wa washiriki hao ulianza kuonekana tokea wakati warembo hao wakiwa kwenye kambi yao ambayo ilifanyika kwenye hotel hiyo ambapo kila mmoja alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuondoka na taji hilo. 

Hali iliendelea kuwa ya mvutano zaidi baada ya baadhi ya washiriki kuaga mashindano hayo na kutoa fursa yaw engine kuingia nafasi ya tano bora katika kinyanganyiro hicho ambacho kilihudhuriwa na wapenzi wengi kuliko kawaida. 

Kitendo hicho kinaonekana kinawezesha kurudisha hamasa na heshima ya shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka mkoani hapa lakini pia kuhamasisha hasa vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki msimu ujao. 

Katika shindano hilo nafasi ya pili ilichukuliwa na Aisha Ally huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Rukaiya Hassani katika shindano hilo ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kusheheni warembo wakali. 

Halikadhalika nafasi ya mrembo kwenye kipaji katika shindano hilo ilinyakuliwa na Edna Chisabo ambapo kinyang’anyiro hicho kilifanyika siku moja kabla ya onyesho la kumsaka mrembo wa mkoa huu kwenye ukumbi wa Tanga City Lounge uliopo mjini hapa. 

Licha ya kufanyika shindano hilo lakini yapo mambo ambayo kimsingi yameweza kuleta msisimuko na kulifanya kuonekana kuwa na ubora wa hali ya juu.  Mambo hayo ndio yamechangia kwa asilimia kubwa kupelekea shindano hilo kuwa na mvuto mkubwa kuliko mashindano mengine ambaye yalikwisha kufanyika mkoani hapa lakini pia uwepo wa watazamaji wengi. 

La kwanza ni eneo ambapo onyesho hilo limefanyika,moja kati ya mambo ambayo yalichangia kuonekana kuwa na mvuta mkubwa ilitokana na shindano hilo msimu huu kufanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort. 

Tunasema hivyo kwa sababu kila mtu anapokwenda kuangalia burudani ya aina yoyote lazima aangalia ulinzi na uimara wa eneo husika hasa ukizingatia wapo baadhi yao huenda na vyombo vyao vya usafiri. 

Kama ujuavyo ulinzi wa mahali husika ndio huwafanya watu kwenda kupata burudani lakini pia ni eneo tulivu ambalowatu wanaweza kufanya mambo yao kila kupata usumbufu wa aina yoyote.  Jambo hilo limesababisha baadhi wa watu kuacha kwenda kwenye maeneo yaliyopo karibu nao na kwenda maeneo mengine ya mbali kwa ajili yakusaka utulivu lakini pia ulinzi. 

Jambo jingine ambalo lilisababisha onyesho hilo kuwa bora ni uwepo wa warembo makini na wenye muonekana bomba na hivyo kupelekea wapenzi na wadau wao kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange huo ambao ulikuwa wa aina yake.
Kilicholifanya shindano hilo kuendelea kuvutia wapenzi na mashabiki ambao walijitokeza ni wasanii ambao walikuwa wakitumbuiza kabla ya kuanza.
Wasanii wanaounda kundi la Nevy Kenzo wazee wa Kamati Chini ilikuwa ni kichocheo kikubwa cha umati mkubwa wa wadau wa tasnia ya urembo na burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano .
Nevy Kenzo ambao walipanda jukwaani kutumbuiza walisababisha ukumbi mzima kulipuka kwa shangwe na nderemo huku baadhi yao wakiimba nyimbo zao ikionyesha namna wanavyokubalika.
Nevy Kenzo wakati akiimba ilifikia wakati mpaka wapenzi na mashabiki wa tasnia ya urembo waliviona viti vyao vya moto na kulazimika kupanda jukwaani kucheza sambamba na wasanii hao.
Haikuishia hapo lakini wasanii ambao walipanda jukwaani kabla ya Nevy Kenzo kutumbuiza wa Kundi la Wazenji Classic lenye makazi yake mjini Tanga walikuwa na moto na kusababisha shangwe kila mahali.
Shangwe hizo zinaonyesha namna kundi hilo lilivyoweza kujizolea
umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanga hasa kwa kipindi kifupi kutokana na aina ya mziki ambao wanaufanya staili ya mduara na bongo fleva.
Sababu kubwa ya kuona kundi hilo kuonekana litakuwa hatari ni namna wanayoweza kulitawala jukwaa wanapokuwa stejini na kuonekana kuinua mara kwa mara wapenzi na mashabiki wao
Suala jingine ambalo lilikuwa kivutio kikubwa ni namna warembo
walivyokuwa wakipanda jukwaani na kuanza kujitambulisha na kujielezea kwa watazamaji.
Hali hiyo ilisababisha wakati mwengine baadhi ya warembo kupanda jukwaani kwa madoido makubwa kwa lengo la kuonyesha umahiri wao ili kuwashawisha majaji kuwapa alama nzuri.
Mbunge wa Jimbo la Tanga atinga Miss Tanga.


Kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)Mussa Mbaruku kuhudhuria shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Tanga mwaka huu kilionyesha namna alivyokuwa kiongozi mpenda michezo na kuithamini.



Mbunge huyo ambaye alikuwa kwenye shughuli zake za kikazi lakini alilazimika kuungana na wakazi wa jimbo lake kumshuhudia mrembo ambaye anapatikana.



Akizungumza mara kabla ya kutangaza mshindi wa Taji la Miss Tanga 2016,Mbunge Mussa alisema tasnia ya urembo imekuwa ikiwapa vijana maisha mazuri lakini pia imekuwa ni daraja la wao kupata mafanikio



Alisema lazima watanzania ikiwemo wazazi kubadilika na kuondokana na dhana ya kuwa ya kuwa urembo ni suala la uhuni kwani imekuwa ikisaidia vijana wengi kupata maendeleo.



"Ndugu zangu lazima tubadilike na kuishi kutokana na utandawazi

uliopo ile dhana ya kuwa urembo ni uhuni mimi nadhani imepitwa na wakati na uhuni mtu anaweza kuwa nao hata asiposhiriki mashindano hayo hivyo wazazi na walezi ruhusuni watoto wenu washiri kwenye mashindano haya "Alisema.



Mussa alisema kuwa anaamini washindi wa shindano hilo wataweza

kuuwakilisha vema mkoa wa Tanga kwenye mashindano ya Kitaifa na kuweza kushinda kama walivyofanya kwenye onyesho hilo.



“Ninaimani kubwa na washindi ambao wamepatikana kwenye shindano hilo wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko kwenye tasnia ya urembo mkoa huu kwani wanaweza hata kuleta taji la Miss Tanzania msimu huu “Alisema.



"Neno la Mshindi wa taji la Miss Tanga 2016 Eligiva Mwasha" Alisema kuwa kwanza anawashukuru wakazi wa Mkoa wa Tanga kwa ujumla kwa sapoti yao walionyesha katika fainali za miss tanga 2016 na yeye kupata fursa ya kunyakua taji hilo



Licha ya kuibuka na ushindi lakini niwaombe niombea kwani kwa sasa safari aliokua nayo bado kubwa sana kwani anamtihani wakwenda kuiwakilisha Tanga katika fainali za Miss Kanda na badae kulekea Katika fainali za miss Tanzania baadae mwaka huu.


No comments:

Post a Comment