Tuesday, August 30, 2016

SHUKRANI ZA FAMILIA YA MAREHEMU MOHAMED MTATURU MKONONGO


Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake
 
Familia ya marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo (pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi, kwa ajali ya gari.


Familia inapenda kuwashukuru kipekee Wakwe wa marehemu - familia ya Mzee Edriss Mavura; Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Prof Elifas T. Bisanda pamoja na uongozi wa chuo na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT);

Uongozi na wafanyakazi wote wa Shirika la Afya duniani (WHO) Uganda na Tanzania; Dr Harvinder Palaha wa Aga Khan Hospital, na madaktari wenzie, wauguzi na wafanyakazi wote wa Aga Khan Hospitali kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU);

Mzee wetu Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi; Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania na Bw. Ziya Kaharan, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki; Prof. Fatmahan Atalar, Mkurugenzi wa MUHAS Genetic Laboratory ya Chuo Kikuu cha Muhimbili; Wanajumuiya wa Ikungi Development Association (IDEA); Umoja wa Wanafunzi waliosoma Uturuki, Masheikh wa Dar es Salaam na Ikungi; na Majirani wote wa Dar es Salaam na Singida.

Kwa kuwa si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja, tunaomba wote mlioguswa na msiba huu mpokee shukrani zetu za dhati.

Tunapenda kuwataarifu kuwa Dua ya arobaini (40) ya marehemu itasomwa Jumamosi, tarehe 03 Septemba 2016, Makiungu-Ikungi, Singida, saa 5 asubuhi Wote mnakaribishwa.






INNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUUN



No comments:

Post a Comment