Friday, July 29, 2016

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI SHAURI LA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA PANGANI


Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso katika akipongezwa na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kutangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kuwa mshindi halali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau






Mbunge Aweso Jumaa akiwa amebebwa juu juu na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kesi iliyofunguliwa dhidi ya mpinzania wake wa CUF Amina Mwidau ya kupinga matokeo ya uchaguzi kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Tanga


Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso wa pili kutoka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Stephen Ngonyani "Proffesa Maji Marefu " wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Tanga wakisuburia kuanzwa kwa kesi hiyo hata hivyo hukumu hiyo ilimpa ushindi halali Mbunge Aweso katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga jana imetupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Pangani lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia tiketi ya CUF Amina Mwindau dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Hamidu Aweso CCM na kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo. 

Akizungumza wakati akitoa huduma ya Shauri hilo,Jaji Patricia Fikirini alisema mlalamikaji Amina Mwindau CUF ameonekana kushindwa katika shauri hilo dhidi ya mlalamikiwa Jumaa Aweso katika upingaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika oct 25 mwaka jana. 

Alisema miongoni mwa malalamiko yalioambatanishwa kutoka kwa mlalamikaji katika zoezi zima la kupinga matokeo hayo ni pamoja na kuwa mlalamikiwa ambae ni Jumaa Aweso katika kampeni zake alikiuka taratibu za uchaguzi,ubaguzi wa mgombea wa jinsia ya kike na kutumia lugha ya siziokuwa za kiungwana jambo ambalo mlalamikaji alidai lilimgharimu kupata matokeo mazuri katika uchaguzi huo. 

Alisema sambamba na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo pamoja na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mlalamikaji havikuwa na ushawishi wa kuweza kutengua matokeo ya uchaguzi huo.
Jaji Fikirini alisema amezingatia hoja zote kutoka pande mbili na kujiridhisha Jumaa Aweso ambae ni mbunge hivi sasa kuwa ni mbunge aliyepita kihalali na hakukuwa na vigezo vya upingwaji wa matokeo aliyopata katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. 

Alisema haki zote za kisheria zipo wazi kwa pande zote mbili mlalamikiwa na mlalamikaji ikiwa pamoja na kukata rufaa kwa maamuzi yaliyochukuliwa na Mahakam hiyo ikiwa kama kuna upande hauta ridhika na hukumu iliyotolewa. 

Kwa upande wake Wakili wa kujitegemea na mahakama kuu Warehema Kibaha alisema Jaji Patisia Fikirini amefanya maamuzi sahihi ya kutenda haki kwa mteja wake katika shauri hilo lililo dumu kwa takriban miezi 7.
Wakili Kibaha alisema katika shauri hilo walijiandaa kwa ushahidi na mashahidi wazuri ili kuweza kukabiliana na kesi hiyo jambo ambaloliliwawezesha kupata ushindi wa kihalali na kuweza kumpa nafasi mteja wake kuendelea na majukumu yake ya Kibunge.
Nae Wakili Mashaka Ngole aliyemsimamia Mlalamikaji Amina Mwindau alisema hana pingamizi lolote na atamsikiliza mteja wake ikiwa ataamua kukata rufaa wataangalia vigezo muhimu vitakavyo wasaidia katika awamu ya pili pindi watakapo kata rufaa hiyo Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso ambaye alikuwa anakabiliwa katika shauri hilo alisema kipindi chote alichokuwa anakabiliana na kesi hiyo kulimpotezea umakinifu wa kufanya majukumu yake ya kibunge na kuweza kuangalia shida za wananchi wa Pangani kwa umakini zaidi. 

Aweso alisema kesi imekwisha na sasa kilichombele yake ni kupambana na kero za wananchi wa Wilaya hiyo ili kuweza kuwaletea maendelo kama alivyowaahidi kipindi cha kampeni.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha


No comments:

Post a Comment