Mratibu Wa watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka WARAMI Ndugu John Marwa kushoto akiwa na Mratibu Msaidizi Makdeo Makeja Kulia wakizungumza na wanahabari mapema leo
Mratibu Wa watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka WARAMI Ndugu John Marwa kushoto akiwa na Mratibu Msaidizi Makdeo Makeja Kulia wakizungumza na wanahabari mapema leo(Habari na picha kwa hisani ya Blog ya Taifa Jema)
WATETEZI WA RASILIMALI WASIO NA MIPAKA (WARAMI)
TAARIFA KWA UMMA.
Ndugu wana Habari,
Tunafuraha kuwafahamisha kuwa sisi ni watanzania tulioamua kuasisi umoja wetu unaotetea rasilimali za nchi, Afrika na Dunia bila kujali mipaka.
Leo tumewaita kuzungumza nanyi kuhusiana na masuala kadhaa yanayoendelea hapa nchini katika kipindi hiki cha serikali yetu pendwa ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli.
1. SAKATA LA SUKARI.
Kama mnavyofahamu sukari ni bidhaa muhimu sana katika maisha ya kawaida ya mwanadamu ya kila siku,
Kama mnavyofahamu pia nchi yetu kwa sasa imeingia katika mgogoro mkubwa wa uhaba wa sukari unaotokana na sababu kadhaa ikiwemo udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa wa bidhaa hiyo muhimu.
Ndugu wana habari, Jana na Juzi vyombo mbali mbali vya habari vimeripoti juu ya mfanyabiashara Zakaria kushirikiana na Mbunge Salim Turki wa mpendae Zanzibar Kuingiza zaidi ya Tani 20,000. Za sukari bila kulipa kodi.
Cha kusikitisha zaidi, Rais amesema hadharani kwamba wafanyabiashara hawa wamekuwa wakinunua Sukari iliyoisha muda wake (expired) na kuja kuibadili mifuko na kuiingiza kwenye mifuko ya hapa nchini na kuiuza bila kujali athari za afya zetu watanzania masikini.
Tunasikitika zaidi kuona Mbunge huyu Turki naye akiwa sehemu ya kufanikisha uharamia huu kama ambavyo magazeti haya yanaonyesha na hakuna hatua zozote za kinidhamu zinazochukuliwa dhidi yake yeye binafsi na wafanyabiashara hawa, zaidi ya yote anapita akitamba mitaani kuwa serikali ameiweka mfukoni na hakuna wa kumfanya lolote, hii ni dharau kubwa sana.
WARAMI inashangazwa na kitendo cha serikali kuchelewa kuitaifisha sukari iliyokamatwa tabata na mbagala ya mfanyabiashara Turki kama ilivyofanya kwa sukari waliyoikamata kule Lindi?, kitu gani kimefichika hapa?.
2. MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA .
ndugu wanahabari,
kwa kipindi kirefu sasa vyombo kadhaa vya habari vimeripoti juu ya baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia vibaya majina ya viongozi ili kufanya biashara na kujimilikisha mali kadhaa.
Mfano hai ni hili tukio la hivi karibuni lililoripotiwa la Mfanyabiashara anayefamika zaidi kama SCABA SCUBA la kupora ardhi za watu maeneo ya kigamboni, kisarawe na mkuranga na wanapomdai na kudai haki zao yeye huwatisha na kuwaonyesha picha za viongozi mbali mbali alizowahi piga nao. HAYA NI MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA.
Mfanyabiashara SCABA tayari anatamba kutumia picha na Rais Magufuli,
Mfanyabiashara huyu anatamba kutumia picha zake na waziri mkuu majaliwa, waziri wa ardhi William Lukuvi, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, mkuu wa wilaya ya temeke Mjema na viongozi wengine kadhaa.
WARAMI inataka kujua uhalali wa mchezo huu wa mfanyabiashara huyu aliyenyang’anya watu ardhi kutumia viongozi je, ni kweli viongozi hawa wamemtuma kufanya hivi?.
Je jeshi la polisi linayafahamu haya?, je haliyaoni haya magazeti yanayoandika hizi habari?, au linapuuzia kwa kuwa wanaodaiwa kuporwa hawana mahusiano ya karibu na viongozi wakubwa wa kitaifa kama ilivyo kwa SCABA SCUBA?.
HITIMISHO
WARAMI inapongeza jitihada zote za dhati anazozifanya Rais Magufuli na Serikali yake za kuhakikisha watanzania tunaishi kwenye usawa, lakini pamoja na hayo tunapendekeza ifuatavyo
i. Jeshi la Polisi na Takukuru waseme ni lini watamkamata Mbunge Turki na kumpeleka mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili?.
ii. Jeshi la polisi na serikali, kwanini wasiichukue sukari iliyokamatwa kwa zakaria na turki na kuigawa kwa watanzania kama walivyofanya kule lindi?.
iii. Tunalitaka jeshi la polisi litoe taarifa rasmi juu ya Mfanyabiashara SCABA anayetamba barabarani kuwa ameliweka jeshi hilo mfukoni na mahakama na kwamba hakuna wa kumfanya lolote katika nchi hii.
iv. Tunazitaka taasisi za kiserikali zifafanue juu ya tabia hii ya wafanyabiashara kutumia picha za viongozi na kuwanyang’anya mali zao, kama ni haki ama si haki.
Imetolewa leo 10.05.2016 na:-
John Marwa
Mratibu WARAMI TAIFA – 0767252990
Makdeo Makeja
Mratibu Msaidizi WARAMI TAIFA - 0789586965
No comments:
Post a Comment