Habari zilizotufikia zinasema kuwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amekuta makontena yenye sukari (115)ikisadikiwa kuwa ni mali ya kampuni ya Mohammed Enterprises. Makonda ameagiza uchunguzi kufanywa ili kujua kwanini sukari hiyo haiko kwenye mzunguko wa biashara au ndiyo ufichaji wa Sukari.
Wakati uchunguzi huo ukiendelea Makonda pia ametaka kujua ubora wa sukari hiyo, kwani amegundua sukari inatengenezwa Brazil wakati packing imefanyika Dubai na kudai kuwa upo uwezekano mkubwa wa uchakachuaji.
Sambamba na hilo eneo jingine amekuta sukari zaidi ya tani (1300) ikidaiwa kuwa ni sukari ya viwandani. Makonda ametoa saa ishirini na nne kupatiwa nyaraka zote, pamoja na TFDA kuhakiki ubora wa sukari hiyo. Mh Makonda amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa swala hili halina chama iwe Ukawa au CCM ikibainika umeficha sukari sheria inachukua mkondo wake ikiwa pamoja na kutaifishwa.
No comments:
Post a Comment