Friday, April 08, 2016

NI MKWAKWANI JUMAPILI HII – Mbeya City Council FC

NYOTA 18 wa kikosi cha Mbeya City Fc sambamba na viongozi 7, alfajiri ya leo, wamewasili salama jijini Tanga tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Mgambo JKT uliopangwa kuchezwa jumapili hii kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Mara baada ya  kuwasiri na kuweka kambi kwenye hotel ya Sea Breeze, kocha mkuu Kinnah Phiri, amezungumza na mbeyacityfc.coma kusema kuwa  wanamshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika salama jijini hapa  hasa baada ya safari ndefu yenye zaidi ya kilomita 900.
Ilikuwa ni safari ndefu, ni kilomita zaidi ya 900 kutoka Mbeya mpaka hapa, wote tuko salama tunamshukuru Mungu kwa kutufikisha katika hali hii, jioni ya leo tutafanya mazoezi kwenye uwanja wa Mkwakwani kwa jili ya kuweka sawa miili yetu pia  kujaribu kuizoea kwa haraka hali ya hewa ya Tanga,  hapa kuna  joto  kubwa  hii ni  tofauti kubwa na kule tulipotoka alisema.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha  utabibu Dk Joshua Kaseko, amethibitisha kuwa hali za wachezaji hao ziko sawa na ataitumia  nafasi ya mazoezi ya jioni ya leo kurejesha  uimara wa misuli ya baadhi ya  nyota ambao kwa namna moja ama nyingine watakuwa  wamepatwa na uchovu mkubwa.
 “Hakuna shaka wote wako sawa, ila nitatumia mazoezi ya jioni  ya leo kama ambavyo programu ya mwalimu inasema ili  kuwaimarisha wale ambao miili yao itakuwa  imepata uchovu  mkubwa kutoka na safari, kuwasili mapema imetusaidia kwa sababu katika hali ya kawaida mchezaji anapwasa apate japo saa 24 za  kupumzika  kabla ya kuingia kwenye mchezo” alisema.
Baadhi ya  nyota walisafiri  kwa ajili ya mchezo huo ni pamoja na Juma Kaseja,Hanningtony Kalyesubula,John Kabanda,Tumba  Lui,Raphael Daud,Kenny Ally,Ditram Nchimbi,Yohana Moriss,Meshack Samwel,John Jerome,Hamidu Mohamed na wengine .


No comments:

Post a Comment