Saturday, March 19, 2016

TPB YAKUTANA NA WAHARIRI KUELEZEA MAFANIKIO ILIYOFIKIA KATIKA MIAKA SITA NA MKAKATI MIPYA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Sabasaba Moshingi, (wapili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF), kutoka kushoto, Makamu mwenyekiti, Deodatus Balile, Mwenyekiti, Theophil Makunga, na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TEF, baada ya kuwakabidhi tuzo za kutambua mchango wa vyombo vya habari katika kuwaelimisha wananchi juu ya huduma zitolewazo na benki hiyo kongwe hapa nchini na kwa kuchaguliwa kwao kuwa viongozi wapya wa TEF. Tukio hili lilifanyika wakati wa hafla ya kila mwaka inayoandaliwa na benki hiyo ya kukutana na wahariri kuzungumzia mafanikio na changamoto za benki hiyo na malengo iliyojiwekea mwaka huu. 
(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
BENKI ya Posta Tanzania, (TPB), imekutana na wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini, na uongozi mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, na kuelezea mafanikio ambayo Benki hiyo kongwe hapa nchini imeyapata katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2016.
Pia Benki hiyo imeeleza mkakati wake mpya wa kuifanya benki hiyo kuwa moja ya mabenki makubwa kabisa sio tu hapa nchini bali nje ya mipaka ya nchi ambapo sasa inatarajia kuwa na jengo lake la kisasa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Ijumaa usiku Machi 18, 2016, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema, mafanikio ya benki hiyo yanatokana na kuweza kuingiza makundi mengi zaidi kufungua akaunti na kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ambapo kila uchao idadi ya wateja wapya inazidi kuongezeka.

Ramani ya Tanzania ikionyesha mtandao wa benki ya posta Tanzania, TPB
Pia alisema, benki hiyo imeziti kutanua mtandao wake kwa kuboresha muonekano wa matawi ya benki hiyo katika mikoa 26 ya bara na visiwani. Alsiema sambamba na matawi hayo huduma za kibenki zinapatikana kote nchini kwenye ofisi za posta.
Makamu mwenyekiti wa TEF, Deo Balile, (kulia), akipokea tuzo yake
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers nchini, TBN, Joachim Mushi, (wakwanza kulia), makamu Mwenyekiti wa TBN, Khadija Kalili, (wanne kushoto), Mmiligi wa K-VIS MEDIA na K-VIS Blog, Khalfan Said, (wakwanza kushoto) na Mhariri Mtendaji wa Business Times/Majira na mmiliki wa ImmaMatukio Blog, Bw. Imma Mbuguni (wapili kushoto)
Moshingi akitoa maelezo ya kina kuhusu huduma za TPB, mafanikio iliyopata na malengo yake ya baadaye
Wahariri wakiwa kwenye hafla hiyo

Moshingi akitoa maelezo ya kina kuhusu huduma za TPB, mafanikio iliyopata na malengo yake ya baadaye
Deo Balile akizungumza kwenye hafla hiyo
Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Guardian, Wallace Mauggo, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mhariri wa biashara wa gazeti la Daily News, Henry Lyimo, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Theophil Makunga akizungumza

Mhariri Mtendaji wa EFM Radio, Scholastica Mazula, akizungumza.
Meneja Mkuu anayeshughulikia masuala ya shirika, na mahusiano ya umma, wa TPB, Noves Moses, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi wa matekelezo na udhibiti majanga, Moses Manyatta(aliyesimama), akizungumza
Moses Nyenyembe, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani
Mkurugenzi wa wateja na biashara, Henry Bwogi
Mkurugenzi wa Teknolojia na Operesheni wa TPB, Jema Msuya
Mkurugenzi wa masuala ya sheria na katibu wa bodi ya TPB, Mystica Mapunda Ngongi
Manyerere Jackton, Mhariri wa gazeti la Jamhuri
Picha ya pamoja
Afisa Mtendaji Mkuu, Sabasaba Moshingi, akiteta jambo na Afisa wa mawasiliano wa TPB, Timotheo Mwakifulefule
Mkurugezni wa fedha wa TPB, Regina Samakafu, akijitambulisha na kuwasalimia wahariri
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akifurahia jambo na wahariri
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo, Joseph Kulangwa na wahariri wenzake wakifuatilia maelezo ya Moshingi
Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali, akiwa makini
Meneja Mkuu wa Manunuzi wa TPB, Anyisile Anywelise, (kulia), akiwasalimia wahariri
Mystica Mapunda Ngongi, akifuatilia kwa makini hoja za wahariri
Saidi Mihiko, Mhariri mwandamizi wa Channel Ten


No comments:

Post a Comment