Monday, March 21, 2016

RAIS MAGUFULI AMPONGEZA DKT.SHEIN KWA KUTEULIWA KUWA RAIS WA ZANZIBAR


 
Rais Dkt.Magufuli pia amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kushiriki Uchaguzi huo kwa amani na utulivu bila kuwepo na kiashiria chochote cha uvunjifu wa amani na hatimaye kumpata mshindi wa kiti hicho cha urais ambayo atawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

"Ninaomba nikupongeze kwa dhati kwa dhati Rais Mteule Dkt.Ali Mohamedi Shein kwa ushindi ulioupata ,ushindi ambao umeonesha kuwa wananchi wa Zanzibar bado wanahitaji uwaongoze tena kwa kipindikingine cha miaka mitano,"anasemaDkt.Magufuli.

Hata hivyo Dkt.John Magufuli ameahidi kuwa Serikali ya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kufanya kazi na kuwataka Wazanzibar kujielekeza katika shughuli za maendelero kwa kuwa uchaguzi umekwisha.
"Ndugu zangu wa Zanzibar Uchaguzi umekwisha,kilichobaki sasa ni kushirikiana na serikali yenu katika kujenga zanzibar yenu na nina imani mna uwezo mzuri wa kuijenga,"anasema.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC),Jecha Salim, leo amemtangaza rasmi Dkt.Ali Mohamedi Shein kuwa mshindi wa kiti cha urais Zanzibar kwa kupata kuwa 299,982 ambayo ni sawa na asilimia 91.4.


No comments:

Post a Comment