Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Lugalema Kahyoza
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akitoa mchango wake kuhusu uboreshaji wa huduma ya Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Lugalema Kahyoza akizungumza na Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es salaam.
Washiriki
wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria
kwa wananchi Februari 1 hadi 3, 2016 katika
viwanja vya Mnazi mmoja, wakifuatilia kikao hicho leo jijini Dar es salaam.
Picha na 4. Mmoja wa
washiriki wa kikao hicho akichangia.
Na. Aron Msigwa
– Dar es
salaam.
Mahakama ya Tanzania imesema
kuwa inaendelea na mkakati wa kufanya maboresho ya miundombinu yake ili
kurahisisha utoaji wa huduma ya mahakama
kwa wadau na wananchi kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein
Katanga wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa
Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3 mwaka huu katika viwanja vya
Mnazi mmoja, jijini Dar es salaam.
Bw. Katanga
amewaambia wadau hao kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya mabadiliko ya
huduma zake kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka Serikalini pia
kutoka kwa wadau wa Haki wanaoiwezesha Mahakama kufanya maboresho hayo kwa
lengo la kukuza Utoaji wa Haki nchini.
Amesema ili kusogeza
huduma karibu na wananchi Mahakama
itatekeleza Mpango mkakati wa miaka 5 wa kuiwezesha kushirikiana kwa karibu
zaidi na wadau na Taasisi za utoaji Haki katika masuala yanayohusu shughuli za kila
siku za utendaji wa Mahakama nchini.
“ Mahakama
tutaanzisha mpango wa miaka 5 ambao utaanzisha mfumo wa wa kushirikiana na
wadau wetu kwa karibu katika mambo yanayohusu shughuli zetu ili kuwaondolea
wananchi usumbufu na upotevu wa muda pindi wanapofuatilia huduma” Amesema.
Amefafanua kuwa
Mahakama imeshaanza kujenga majengo mapya ya kisasa ya Mahakama za Mwanzo
katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mahakama
ya mwanzo Kigamboni jijini na Kawe zote za jijini Dar es salaam, Mahakama ya Wilaya
ya Mkuranga na Kibaha mkoani Pwani ili
kurahisisha utoaji wa Haki.
“ Mahakama sasa tuko
katika mwelekeo mzuri wa kufanya mabadiliko, kwa kushirikiana na wataalam wetu
wa ndani wakiwemo Chuo Kikuu Ardhi , tunaendelea kujenga majengo mapya ya
Mahakama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mahakama ya Mwanzo Kigamboni,
Mkuranga, Kibaha na Kawe ambayo yatakamilika ifikapo Juni mwaka huu”
Amesisitiza.
Bw. Katanga ameongeza
kuwa mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa majengo yaliyopo yanakarabatiwa sanjali
na ujenzi wa majengo mapya katika Mahakama zote 133 nchi nzima.
Aidha, amebainisha
kuwa Mahakama inaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa watumishi wake ikiwemo
ununuzi wa mabasi ya kusafirishia watumishi, magari madogo na Pikipiki ili
kuwawesha watumishi wa Mahakama kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Solanus Nyimbi akizungumza na wadau hao amewataka
wafanye kazi kwa kushirikiana katika kuwahudumia wananchi ili kuongeza imani
yao kwa Mahakama.
Amezitaka Taasisi na
wadau wanaohusika na utoaji wa Haki kujikita katika kushughulikia matatizo ya
wananchi ili kufanikisha dhana ya Utoaji Haki kwa Wakati ili kwenda na mpango
uliowekwa na Mahakama wa kuondoa mrundikano wa mashauri mahakamani na ule wa
kuzifuta kesi zilizokaa muda mrefu.
Naye Msajili wa Mahakama
ya Rufaa, John Lugalema Kahyoza ametoa
wito kwa Taasisi za Utoaji wa Haki kukutana mara kwa mara ili kujdili na
kutatua changamoto zinazoukabili Utoaji wa Haki nchini.
No comments:
Post a Comment