Star huyo wa tamthilia halisi, ameweka picha yake akiwa mtupu kama alivyozaliwa kwenye mtandao wa Twitter. Picha hiyo imeleta hisia tofauti kwa watumiaji wa mitandao, wengi wakipiga vita hatua hiyo na kudai inahamsha hisia zao.
Lakini ofa hiyo ya Kim, sio ya kushangaza sana kutokana na tabia yake. Si mara ya kwanza kumuona Kim akiwa katika vazi lake la kuzaliwa, sasa ni kipi cha ajabu leo. Mwili wake ndio kipato chake, anachokifanya kwa kiasi kikubwa kinamhusu yeye.
Kuna baadhi ya wanawake hujisikia na kujiamini zaidi wanapokuwa uchi, wengine kwa kupinga lakini hakuna mwenye ubavu wa kumzuia mwingine kufanya hivyo.
Kama tunalenga kuwasaidia watoto wetu na vijana wadogo kuweka malengo mazuri, kuwa na afya bora na kuwa mfano bora kwa jamii, inatulazimu tuangalie ndani ya nyumba zetu kwa makini zaidi na kuweka mazingira sahihi kupigana na tabia hizo.
Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la nchin Uingereza,Daily Mail, mwaka jana pekee, zaidi ya vijana wadogo 60,000 walijipiga picha za uchi (Selfie), na kuweka kwenye internet, picha hizo ziliondolewa katika mitandao na taasisi ya uangalizi wa internet.
Tunahitaji hatua kama hizo kwenye jamii yetu nchini Tanzania, kesho sintoshangaa kusikia wasichana nchini wakijinadi miili yao kwa mtindo huo. Mbaya zaidi tunaamini kuwa utamaduni sahihi ni ule wa Marekani na kupuuza wa kwetu ambao humuandaa na kumjenga kijana kuwa mtu bora na mwenye maadili mema kwa jamii yake.
Tukumbuke sio kila utamaduni ni wa kuiga, tuchukue mema tuache maovu
No comments:
Post a Comment